Wednesday 15 July 2015

UKAWA BADO NGOMA NZITO

By    
KITENDAWILI cha nani atakuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya kambi ya upinzani katika uchaguzi mkuu wa baadaye mwaka huu, jana kilishindwa kupata jibu baada vyama vinavyoundwa kambi hiyo, kukutana kuanzia asubuhi hadi usiku, lakini bila ya kukubaliana.

Hali hiyo inaelezwa imetokana na kushindwa kuafikiana katika hoja kadhaa za msingi, kabla ya kuridhia kumtangaza mgombea wa umoja huo.

Aidha, katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, mmoja wa wenyeviti wa vyama vinavyounda umoja huo, ambaye pia ni mmoja wa waliojitokeza akiomba kupendekezwa awe mgombea, Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF, hakutokea.

Wakati Profesa Lipumba akikosekana, viongozi wengine wa juu wa Ukawa waliokuwepo akiwamo Freeman Mbowe wa Chadema, James Mbatia wa NCCR Mageuzi na Dk. Emmanuel Makaidi wa NLD.

Wengine waliokuwepo kwenye kikao hicho ni wagombea nafasi ya urais walioteuliwa na vyama vyao ili kuchuana ndani ya Ukawa na kupata mgombea mmoja atakayewakilisha kundi hilo.

Hao ni Dk Willibrod Slaa na Dk George Kahangwa wa NCCR. Mgombea atakayepitishwa na umoja huo, atachuana na mgombea wa CCM, Dk. John Magufuli.

Chanzo: Habari leo

0 comments