Tuesday 1 September 2015

DR. SLAA AACHANA NA SIASA, AMCHANA LIVE LOWASA NA SUMAYE

By    
Aliyekuwa Katibu mkuu wa Chadema, Dr. Wilbord Slaa akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam
Aliyekuwa katibu mkuu wa Chadema Dr. Wilbert Slaa leo ametangaza kuachana na siasa za vyama, na sasa atakuwa mpambanaji wa haki za wanyonge bila kujihusisha na chama chochote kile.

Dr. Slaa amesema hayo leo pale alipokuwa anaongea na waandishi wa habari juu ya ukimya wake wa takribani mwezi mmoja, na kuzushiwa taarifa nyingi, ambazo ndani yake kuna ukweli na upotoshwaji.

Dr Silaa alitumia muda mwingi kuizungumzia sakata laMgombea uraisi wa Chadema Edward Lowasa, huku akieleza viambatanisho vinavyo mtuhumu Lowasa kuwa fisadi na afai kuwa raisi wa nchi hii.

Dr. Slaa alieleza kuwa hakuwa na dhamira ya kugombea urasis kwa kivuli cha Ukawa kupitia Chadema, na kuwa yeye alihusika katika majadiliano ya mwanzo ya kumpokea Lowasa ndani ya Chadema baada ya kukatwa na CCM.

Dr Slaa alisema kuwa yeye alitoa masharti kwa Lowasa, ambayo alitakiwa kuyatekeleza kabla ya kuwa mwanachama wa Chadema ambapo alishindwa kufanya hivyo na yeye kujitoa katika mchakato mzima.

Dr. Slaa alimfafanua Lowasa na wanachama wengine wa CCM waliojiengua CCM na kuingia Chadema kuwa ni Makapi ya CCM, na kuingia kwao Chadema kumepelekea Chama hicho kutoka katika misingi yake.

Katika mazungumzo yake na waandishi wa Habari Dr Slaa alifafanua udhaifu wa Lowasa na Sumaye na kuonyesha namna gani walivyo kuwa waongo.

0 comments