
Aidha, nauli ya mwanafunzi itakuwa kati ya Sh. 250 na 450 kwa safari moja, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), imetangaza jana.
Tangazo la Sumatra kwa vyombo vya habari jana lilieleza kuwa, mamlaka hiyo imepokea maombi ya nauli kutoka kwa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (Udart) ambao utatoa huduma ya usafiri wa umma katika kipindi cha mpito.
Tangazo hilo lilieleza kuwa, safari katika njia kuu pekee mathalani Kimara Mwisho hadi Kivukoni itakuwa Sh. 700 kwa mtu mzima wakati nauli ya mwanafunzi itakuwa Sh. 350. Hivyo kwenda na kurudi kwa mtu mzima itakuwa Sh. 1,400 na mwanafunzi itakuwa Sh. 700.
Aidha, nauli ya pembezoni (Mbezi hadi Kimara Mwisho), itakuwa Sh. 500 kwa mtu mzima wakati kwa mwanafunzi itakuwa Sh. 250.
Pendekezo lingine la nauli ni kwa abiria watakaopita njia ya pembezoni na kisha njia kuu kama kutoka Mbezi-Kimara Mwisho hadi Kivukoni, nauli itakuwa Sh. 800 kwa mtu mzima wakati kwa mwanafunzi itakuwa Sh. 400.
Safari nyingine ni kwa abiria wanaotumia njia ya pembezoni, njia kuu halafu njia ya pembezoni. Mfano wa safari hiyo ni wanaotoka Mbezi-Kimara Mwisho hadi Morocco; nauli yao itakuwa Sh. 900 na wanafunzi itakuwa Sh. 450.



0 comments