Friday 2 October 2015

UNESCO YAENDELEA KUZIJENGEA UWEZO REDIO ZA JAMII NCHINI

By    
1
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph, akizungumza katika kongamano lililowakutanisha watendaji kutoka Redio za jamii nchini katika mji wa Terat, wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara jana.
2
Mwenyekiti wa Muungano wa Redio za Kijamii nchini (COMNETA), Sekiku Joseph akizungumza katika Kongamano hilo ambalo amesisitiza umuhimu wa viongozi wa Radio za kijamii kuthamini michango inayotolewa na wafadhili ili iweze kuwa endelevu.
3
Mshauri na Mkufunzi wa masuala ya vyombo vya habari jamii kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akisistiza jambo katika mafunzo hayo.
4
Afisa Miradi mpya wa Unesco, Nancy Kaizirege akisisitiza jambo.
5
Mkurugenzi wa Redio ya Jamii Uvinza FM, Ayub Kalufya akichangia mada na kuomba Unesco kuendelea kutoa usaidizi kwao kutokana na mchango wanaoutoa kwa jamii.
6
Afisa Miradi mpya wa Unesco, Nancy Kaizirege akisisitiza jambo wakati mafunzo hayo yakiendelea. kulia ni Meneja wa Orkonerei Radio Service Simanjiro Manyara (ORS FM), Bw.Baraka Ole Maika.
7
Mwenyekiti wa Bodi ya Redio ya Jamii 94.9 FM , Mkoani Pemba, Hamidu Hassan Bakari akizungumza namna Redio yake itakavyonufaika kupitia mafunzo ya kuwajengea uwezo na vifaa ya matangazo.
8
Meneja wa Redio Kahama FM, Marco Mipawa, akizungumza jambo.
Mwandishi Wetu,Simanjiro
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,Sayansi na Utamaduni(UNESCO) limeendelea kuimarisha Redio za Jamii nchini kwa kuwapa mafunzo ya mara kwa mara watendaji wa ngazi mbalimbali kwa lengo la kuzifanya Redio hizo kuwahudumia vema wananchi wanaoishi maeneo ya vijijini.
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph amesema kumekuwa na mafanikio tangu mradi huo kuanza miaka mitatu iliyopita chini ya ufadhili wa UNESCO, Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) na Serikali ya Uswizi ambapo licha ya kuwajengea uwezo vifaa vya kieletroniki vilitolewa kwa Redio hizo.
Kongamano hilo la mwaka la siku tatu(3) linafanyika katika Kituo cha Orkonerei Radio Service Simanjiro Manyara (ORS), Terat wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara na limewaleta pamoja watendaji wa Redio za Jamii 20 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar .
“Tunalenga kuwajengea uwezo ili hizi Redio za Jamii zifanye kazi kwa weredi ya kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi waweze kushiriki mijadala inayohusu sekta za afya, elimu na kilimo,”amesema Yusuph
UNESCO inafanya kazi kwa karibu na Muungano wa Radio za Kijamii Tanzania(COMNETA)unaongozwa na Mwenyekiti wake Sekiku Joseph.

0 comments