Tuesday 10 November 2015

NIMEITOA KWA ZITTO "RAISI WANGU MWANAOXALATO (Dr John Pombe Magufuli) JARIBIO LINGINE LILIOPO MBELE YAKO NI KWENDA BUNGENI NA PENDEKEZO LA KUFUTA SITTING ALLOWANCES ZA WABUNGE WETU:"

By    

Zitto Kabwe

Kwa takribani muongo mzima sasa vyama vya upinzani vimekuwa mstari wa mbele kupigia kelele suala matumizi mabovu yanaofanywa na serikali ikiwemo suala la ulipaji wa posho za vikao (sitting allowances) kwa viongozi mbalimbali waandamizi wa serikali wakiwemo wabunge. 

Kwa bahati mbaya sana wengi wao (vyama vya upinzani) wamekuwa wakijivika sura ya uzalendo na kutangaza hadharani kutokuwepo kwa mantiki ya wao kulipwa posho ili hali wamekuwa wakizunguka mlango wa nyuma kuzikusanya posho husika. 

Na kama haitoshi wengi wamekuwa wakihudhuria vikao vingine vya taasisi na wizara mbalimbali za serikali na huko pia wamekuwa wakikusanya posho kama kawaida yao, kadhalika tumeshuhudia wabunge mbalimbali ambao ni wajumbe wa bodi wa mashirika ya uma pamoja na kamati wamekuwa wakilazimisha kuhudhuria vikao mbalimbali vya kitaalamu na wamekuwa wakishinikiza kulipwa posho tena kwa viwango wavitakavyo wao.

Binafsi nimefurahishwa sana na uamuzi wako wa kufuta safari zote na malipo ya posho kwa ajili ya vikao ya watumishi wa uma (sitting allowances). 

Ili tusiwe na double standards juu ya uamuzi huu sasa ni wakati muafaka wakati unalihutubia bunge Mhe Raisi kulitangazia bunge letu tukufu azima yako ya kupunguza matumizi yasiokuwa yalazima serikalini ikiwemo suala la kufuta posho za wabunge na wabakie kupata mishahara tu kama watumishi wengine ambao hatuna hizi posho. 

Hili lifanikiwe vizuri ni kutumia approach ya divide and rule kwa kulipeleka bungeni kama pendekezo (mtengo) na kisha wao wenyewe wajipime waone kama wanastahili kuendelea kulipwa au wasitishiwe. 

Na hapo ndipo tutawajua wanafiki na wazalendo wa kweli kwa nchi yetu. Ni muhimu tuyaishi maneno yetu kwa vitendo kama ambavy mmoja ya wabunge wa upinzani ZZK amekuwa akihubiri siku zote.

Usife moyo watanzania tuko nyuma yako, tuna kuunga mkono kwa hali na mali katika jitihada zako za kuwatumikia watanzania kwa moyo wote.

Ni mimi Mtanzania Mwanaoxalato.

0 comments