Thursday, 19 November 2015

PSG KUVAA JEZI MAALUM KUOMBOLEZA SHAMBULIZI LA KIGAIDI LA UFARANSA

By    
Mabingwa wa Ufaransa, Paris Saint-Germain watavaa jezi maalum zinazotoa pole ikiwa ni sehemu ya kuonyesha wanaombeleza lile tukio la magaidi walioshambulia jiji la Paris.


Magaidi walishambulia maeneo mbalimbali ya Paris na kuua watu 129.

Hali hiyo ilizua hofu katika maeneo mbalimbali ya Paris na Ufaransa yote, pia nchi jirani.

Lakini shambulio hilo lilisababisha hofu hadi katika michezo kutokana na washambuliaji watatu kujiripua nje ya Uwanja wa soka wakati Ufaransa ikicheza na Ujerumani, mechi ya kirafiki.

0 comments