Thursday 10 December 2015

MAGUFULI ATEUA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI

Leo Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dr John Magufuli anatangaza baraza la mawaziri wa Jamhuri wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Tuwe pamoja kulifahamu baraza letu.

Magufuli: Kumekuwa na speculation nyingi na watanzania wamekuwa na hamu kubwa ya kujua baraza la mawaziri, baada ya kusubira kwa muda mrefu, baada ya kuapa tulitakiwa angalau tarehe kumi tuwe tumetangaza baraza. 

Tuliona angalau tujiridhishe kwanza, baraza lililopita lilikuwa na mawaziri na manaibu zaidi ya 59, tukaona tuwe na baraza dogo. Hatuwezi kukaa bila baraza, katika baraza hili, wizara nyingi tumeziunganisha na kutakuwa na wizara 18 na tutakuwa na mawaziri 19 tu, kuna baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na manaibu waziri. 

Lengo ni kutimiza ahadi yetu ya kuwa na baraza dogo kupunguza gharama na effective kwa kufanya kazi. Zilitengwa bilioni 2, mawaziri watakapoteuliwa waende semina elezi, baraza nitakaloliteua halitakuwa na semina elekezi na fedha tutaelekeza sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure. Watafanya semina elekezi wenyewe ndani kwa ndani.

WIZARA
Ofisi ya Rais, Tamisemi, utumishi na utawala bora: Mawaziri ni George Simbachawene na Angela Kairuki, Naibu waziri Jaffo Selemani Said

Ofisi ya makamu wa Rais, muungano na mazingira: Makamba na naibu wake ni Mpina

Ajira, walemavu: Jenista Mhagama, Naibu nimemtua mbunge, Pos Abdallah ambae ni mhadhiri Dodoma

Ulemavu: Waziri ni Anthony Mavunde

Kilimo, mifugo na uvuvi: Waziri ni Mwigulu Lameck Nchemba, Wiliam Nashe naibu waziri

Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano: Waziri bado sijamtafuta, naendelea kumfikiria, Naibu waziri Edwin Ngonyani.

Fedha na mipango: Waziri bado tunamtafuta, naibu waziri ni Kijachi

Nishati na madini: Waziri ni Professa Muhongo, Naibu waziri ni Medadi

Katiba na sheria: Waziri Harisson Mwakyembe

Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki: Waziri ni Augustino Mahiga ambae nimemteua kuwa mbunge na kisha waziri, Naibu ni Dr Suzan Kolimba.

Ulinzi na kujenga taifa: Waziri ni Dr. Hussein Mwinyi

Wizara ya mambo ya ndani: Charles Kitwamba

Ardhi na maendeleo ya makazi: Waziri ni Wiliam Lukuvi, Naibu Angelina Mabula

Maliasili na Utalii: Waziri bado, naibu ni Ramo Makala

Viwanda na biashara: Waziri Charles Mwijage

Elimu, Sayansi na ufundi: Waziri bado hajapatikana, Naibu ni Stella Manyanya

Afya, maendeleo ya jamii na Ustawi wa jamii: Ummy Mwalimu, Naibu ni Hamis Andrea Kingwangala

Habari, utamaduni, wasanii na michezo: Nape Nnauye, naibu Anastazia Wambura

Wizara ya maji na umwagiliaji: Makame Mbarawa ambae nilimteua kuwa mbunge, Naibu ni Kamwene

0 comments