 Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo akizungumza katika
 hafla ya kukabidhi hundi ya ushuru wa huduma kwa halmashauri ya mji wa 
Kahama, hafla hiyo ilifanyika baada ya kukamilika kwa hafla ya kukabidhi
 madarasa ya shule ya
 msingi Budushi na nyumba za walimu Mwime.
  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo akizungumza katika
 hafla ya kukabidhi hundi ya ushuru wa huduma kwa halmashauri ya mji wa 
Kahama, hafla hiyo ilifanyika baada ya kukamilika kwa hafla ya kukabidhi
 madarasa ya shule ya
 msingi Budushi na nyumba za walimu Mwime.  Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama wakishuhudia wakati wa hafla ya makabidhiano ya hundi
 Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama wakishuhudia wakati wa hafla ya makabidhiano ya hundi  Mbunge wa Kahama Mjini Mhe. Jumanne Kishimba akihutubia wananchi wa 
Kahama wakati wa kupokea hundi ya ushuru wa huduma yenye thamani ya 
zaidi ya shilingi milioni 700
 Mbunge wa Kahama Mjini Mhe. Jumanne Kishimba akihutubia wananchi wa 
Kahama wakati wa kupokea hundi ya ushuru wa huduma yenye thamani ya 
zaidi ya shilingi milioni 700  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi,Asa Mwaipopo akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu wakati wa makabidhiano ya hundi ya malipo ya huduma.
 Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi,Asa Mwaipopo akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu wakati wa makabidhiano ya hundi ya malipo ya huduma.   Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akihutubia wananchi wa Kahama wakati wa kupokea hundi ya ushuru wa huduma
  Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akihutubia wananchi wa Kahama wakati wa kupokea hundi ya ushuru wa huduma
Na Dixo Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.
Mgodi
 wa Buzwagi umekabidhi wa halmashauri ya mji wa Kahama hundi yenye 
thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia saba na kumi na saba 
(717,276,055/=) ikiwa ni sehemu ya malipo
 ya kodi ya huduma(service levy) ambayo hulipwa kwa halmashauri hiyo.
Akizungumzia
 malipo hayo ya hundi Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa 
Mwaipopo amesema kiasi hicho ni malipo ya kuanzia mwezi januari hadi 
juni mwaka huu.
Mwaipopo
 ameongeza kuwa licha ya Kampuni yake kulipa kodi mbalimbali na 
kujishughulisha katika kufadhili miradi ya Maendeleo, amesema ipo haja 
ya Jamii kuilinda na kuitunza miradi hiyo ili iwe na
 manufaa kwa Jamii nzima.
“Acacia
 kupitia Mgodi wetu wa Buzwagi tunajivunia kuwa wadau muhimu wa 
maendeleo wa halmashauli ya mji wa Kahama na serikali kwa ujumla, na 
tunafarijika sana kwa ushirikiano ambao tumekuwa tukiupata,
 ombi letu kwa Jamii zinazonufaika na miradi yetu kuilinda na kuitunza kwa manufaa ya Jamii nzima.”
Kwa
 upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Fadhili Nkurlu aliyepokea hundi ya kodi ya huduma kutoka kwa uongozi wa 
Mgodi wa Buzwagi na baadae kuikabidhi kwa mwenyekiti wa halmashauri
 ya Kahama ameupongeza uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kwa jitihada ambazo 
wamekuwa wakizifanya katika kuhakikisha wanashirikiana na jamii katika 
kutekeleza miradi ya Maendeleo”
Akizungumza
 kwa niaba ya halmashauri ya mji wa Kahama Mwenyekiti wa halmashauri 
hiyo Abel Shija ameupongeza uongozi wa Mgodi na kuahidi kuendelea 
kushirikiana nao katika kuiletea Jamii Maendeleo.
Mwisho. 
 



 
  
 
 
 
0 comments