Wednesday 4 October 2017

MBUNGE CHUMI AZIPIGA TAFU TIMU ZA JIMBONI KWAKE KWA KUZIPA VIFAA VYA MICHEZO NA FEDHA

Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akitoa maelezo wakati wa kugawa vifaa vya michezo kwa timu za mafinga mjini pamoja na kuisaidia timu ta Mufindi United kiasi cha shilingi laki Tano
Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akipeana mkono na viongozi wa timu ya Mafinga veterani wakati wa kugawa vifaa vya michezo kwa timu za mafinga mjini pamoja na kuisaidia timu ta Mufindi United kiasi cha shilingi laki Tano


 Na fredy Mgunda, Mafinga

Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi amezipiga tafu timu zinazoshiriki ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa wa Iringa kwa kuzipatia jozi moja moja ya jezi kwa kila timu lakini pia ameichangia timu ya Mufindi United inayoshiriki lingi daraja la kwanza Tanzania bara kiasi cha shilingi laki tano kwa lengo la kuisaidia katika harakati zake za kupanda daraja.
 
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa na pesa hizo Chumi alisema kuwa ameguswa kufanya hivyo kwa kuwa anapenda michezo na anacheza mpira wa miguu kufanya hivyo kutaendelea kuzipa morali timu za jimbo la Mafinga Mji kufanya vizuri kwenye mashindano wanayoshiriki.
  

"Leo nimekabidhi jezi kwa timu zinazoshiriki daraja la tatu ngazi ya mkoa na timu hizo ni Bajaji Fc,Mabo Fc (Boda Boda) na Kinyanambo United nimefanya hivyo kuzifanya timu hizi kuzihamasisha kufanya vizuri kwenye ligi hiyo" alisema Chumi


Chumi aliwataka wananchi na wadau wanaoipenda timu ya Mufindi United kuendelea kuisaidia katika haraka za kupanda daraja kwa kuwa kuendesha timu ni gharama kubwa hivyo tuungane kwa pamoja kufanikisha lengo letu ili kupata timu itayokuwa ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao.


“Jamani kushiriki ligi daraja la kwanza ni gharama sana na ligi ya mwaka huu ni ngumu hivyo tunahitaji kuwa na pesa nyingi kufanikisha lengo letu la kuwa na timu ya ligi kuu wenzetu wengine wamejipanga sana na wanapesa hivyo timu yetu ikiwa na njaa itatuwia vigumu kuipandisha” alisema Chumi


Aidha Chumi hakusita kuwapongeza viongozi wa timu ya Mufindi United pamoja na mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William kwa kuendelea kuisadia timu kushiriki lingi hivyo kwa michango na mawazo yao.


“Mimi nilijua mwaka huu tunashushwa daraja maana hali ilikuwa ngumu wakati wa usajili lakini viongozi hawa walipigana kufa na kupona wakahakikisha timu inasajili na inacheza ligi hiyo” alisema Chumi



0 comments