Thursday, 8 March 2018

BOHARI YA DAWA (MSD) YAZIDI KUBORESHA HUDUMA ZAKE YATAMBULIKA KIMATAIFA

By    
 Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana walipotembelea Bohari ya Dawa kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na bohari hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Ugavi, Byekwaso Tabula, akitoa maelezo kwa wanahabari jinsi vifaa tiba na dawa zinavyohifadhiwa katika bohari hiyo.
 Muonekano wa maboksi ya dawa jinsi yalivyopangwa ndani ya bohari iliyopo Makao Makuu ya MSD Keko jijini Dar es Salaam.
 Dawa na vifaa tiba zikipelekwa kuhifadhiwa ndani ya bohari.
 Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu, akiwaonesha waandishi wa habari vifaa  mfuko wenye vifaa vya kujifungulia akina mama (Delivery Pack). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Ugavi, Byekwaso Tabula na Kaimu Mkurugenzi  Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda, Salome Malamia.
  Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu, akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
 Kaimu Mkurugenzi  Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda, Salome Malamia, akiwaonesha wabahabari vifaa vilivyopo kwenye mfuko huo.
 Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu, akimkabidhi mfuko wenye vifaa hivyo mwandishi wa habari, Hilda Mhagama kutoka  gazeti la Daily News.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu, akimkabidhi mfuko wenye vifaa hivyo mwandishi wa habari, Saum Juma kutoka Kituo cha Televisheni cha TV One.

Na Dotto Mwaibale

BOHARI ya Dawa (MSD) imezidi kuboresha huduma zake za Ununuzi, Utunzaji na Usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara hata kukidhi viwango vya ubora wa Kimataifa na kupata ithibati ya ISO 9001:2015.         

Akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari  Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu ameeleza kuwa kampuni ya Kimataifa ya ACM LIMITED ilifanya ukaguzi Makao makuu ya MSD pamoja na Kanda zake nane mwezi Agosti 2017 na MSD ilionekana kufuata miongozo ya juu ya kimataifa na matakwa ya mamlaka za udhibiti ubora nchini.             

Katika mkutano huo, Bwanakunu pia alieleza kuwa hali ya upatikanaji wa dawa muhimu(135)  MSD imeimarika  na kufikia asilimia 90,huku kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini hali ya upatikanaji wa dawa ni kati ya asilimia 85 na 98.              

Mkurugenzi Mkuu wa MSD pia aliwaonyesha waandishi wa habari  Mfuko wenye vifaa vya kujifungulia akina mama (Delivery Pack) ambao umepunguzwa bei kutoka shilingi 40,000 mpaka shilinhi 21,000.

Amesihi taasisi, asasi, jumuiya na wananchi kununua mifuko hiyo ya vifaa vya kujifungulia na kutoa msaada kwenye vituo vya afya na hospitali ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha huduma za afya nchini .      
                              
Katika mkutano huo Bwanakunu aliwazawadia waandishi wa habari wawili ambao ni wajawazito mfuko huo wa vifaa vya kujifungulia  kwa ajili ya kujiandaa kwenda kujifungua.

0 comments