Katika hali isiyokuwa ya kawaida kijana mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Maneno amefanya kituko cha kushangaza baada ya kupanda juu ya mnara wa simu za mkononi hadi kileleni na kukaa kwa muda wa saa 9 bila msaada wowote wa uokozi kutoka mamlaka husika.
Wakizungumza na Azam TV baadhi ya mashuhuda waliozungumza naye akiwa Juu wamedai kuwa amechukua uamuzi huo kwa madai kuwa amesikia taarifa kwenye vyomba vya Habari kuwa, Edward Lowasa amehukumiwa kifungo jela, taarifa ambazo si za kweli, bali ni taarifa ya ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ambaye amehukumiwa kifungo za miezi 5 jela.
Akidhibitisha kutokea Kwa tukio hilo Mwenyekiti Wa Kijiji cha Mtakuja Kata ya Buseresere Wilaya ya Chato mkoani Geita, Varely Kakonko amedai kuwa kijana huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 24-26 ni mwenye matatizo ya akili na jaribio hilo siyo la kwanza kutokea kwani awali alishawahi kufanya jaribio kama hilo la kupanda kwenye moja ya minara ya simu za mkononi.
Kijana huyo amekaa katika kilele cha mnara huo zaidi ya saa 9 hadi alipoamua kushuka kwa hiari yake majira ya saa 12 jioni ambapo tayari jeshi la Polisi kwa kushirikiana Jeshi la Zimamoto na Uokozi walimchukua mtu huyo hadi Kituo cha Buseresere kwa uchunguzi zaidi.
CHANZO : ukurasa wa facebook wa Azam TV

0 comments