Naibu waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara katika Kitongoji cha Mahiga, Kijiji na Kata ya Mwakitoliyo, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kusikiliza kero za wananchi hao, Juzi 11 Machi 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Wakazi wa Kitongoji cha Mahiga, Kijiji na Kata ya Mwakitoliyo, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakimsikiliza Naibu waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb) wakati wa mkutano wa hadhara, Juzi 11 Machi 2018.
Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe Ahmed Salum akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo kabla ya kumaribisha Naibu waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb) kusikiliza kero za wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika Kitongoji cha Mahiga, Kijiji na Kata ya Mwakitoliyo, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Juzi 11 Machi 2018.
Naibu waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb) akiwatuliza wananchi wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika Kitongoji cha Mahiga, Kijiji na Kata ya Mwakitoliyo, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ili kusikiliza mgogoro baina ya wananchi hao na kampuni ya Henan Afro-Asia Geo Engineering co ltd kutoka nchini China, Juzi 11 Machi 2018
Naibu waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb) (Kushoto) akisikiliza malalamiko kwa baadhi ya Wakazi wa Kitongoji cha Mahiga, Kijiji na Kata ya Mwakitoliyo, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kabla ya mkutano wa hadhara uliofanyika Juzi 11 Machi 2018.
Na Mathias Canal,
Shinyanga
Serikali imekiri kuwepo kwa changamoto katika ulipaji wa fidia
kwa wananchi waliofanyiwa uthamini katika maeneo yao ili kupisha mradi wa
uchimbaji wa madini ya dhahabu kupitia kampuni ya Henan Afro-Asia Geo
Engineering co ltd kutoka nchini China.
Akizungumza Juzi 11 Machi 2018 na wananchi waliojitokeza kwenye
mkutano wa hadhara katika Kitongoji cha Mahiga, Kijiji na Kata ya Mwakitoliyo, Halmashauri
ya Wilaya ya Shinyanga, Naibu Waziri wa wizara ya madini Mhe Doto Mashaka
Biteko (Mb) amekiri kuwa zipo changamoto katika jambo hilo hivyo serikali
itapitia upya tathimini sambamba na ulipaji wa fidia ili kuhuisha sintofahamu
hiyo iliyopelekea wananchi hao kupaza sauti zao za malalamiko.
Mhe Biteko alisema kuwa katika sekta ya madini mnufaika wa kwanza
lazima awe mtanzania kwani sheria ya madini ya mwaka 2010 iliyofanyiwa
marekebisho mwaka 2017 inaelekeza kuwa na uchumi fungamanishi kwa wananchi ili
kuinua pato la wananchi sambamba na mchango wa sekta ya madini kwenye Pato la
Taifa.
Aidha, Mhe Biteko aliwasihi wananchi hao kuwa watulivu katika
kipindi kifupi ambacho serikali inapitia upya tathmini hiyo huku akiwasihi
kuacha uvamizi katika eneo hilo kwani kufanya hivyo ni uvunjifu wa sheria,
kanuni na taratibu za nchi.
“Ndugu zangu wananchi Sio kweli kwamba wawekezaji ni wabaya lakini
wanapaswa kutambua tu wakija kuwekeza nchini wanapaswa kufuata sheria, kanuni
na taratibu za nchi ikiwa ni pamoja na kuwa na mahusiano mazuri na wananchi
wanaoishi karibu na mradi huo” Alikaririwa Biteko (Mb)
Machi 10,
2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli
akihutubia mamia ya wananchi katika
eneo la Nyasubi katika Halmashauri ya mji wa Kahama Mkoa wa Shinyanga wakati wa dhifa ya uzinduzi wa barabara
ya Isaka-Ushirombo yenye urefu wa Kilomita 132, alimuagiza Naibu Waziri wa wizara ya madini Mhe Doto
Mashaka Biteko (Mb) kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe Ahmed Salum kufanya
ziara na kuwasikiliza wananchi kuhusu malalamiko hayo ili serikali kutafuta
ufumbuzi wa haraka.
Wananchi hao wanalalamikia kufanyiwa tathmini tofauti na matakwa
ya sheria huku wakipatiwa malipo kiduchu pasina kufanyika mkutano wa hadhara wa
maridhiano baina ya wananchi na muwekezaji huhu wakiomba kufanyika upya
tathmini ya maeneo yao.
MWISHO
0 comments