Tuesday, 13 March 2018

MNEC SALIMU ASAS ATOA SHILINGI MILIONI KUMI NA TATU (13,000,000) KWA AJILI YA MAENDELEO YA UWT IRINGA MJINI

By    
 Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas akiongea na wajumbe wa baraza la UWT manispaa ya Iringa lilofanyika katika ukumbi wa CCM sabasaba na kutoa jumla ya shilingi milioni
kumi na tatu(13,000,000) kwa UWT Iringa Mjini
 Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas akipokea zawadi kutoka kwa viongozi wa UWT manispaa ya Iringa
 Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas akibadilisha mawazo na mwenyekiti wa UWT manispaa ya Iringa Ashura Jongo pamoja na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

MJUMBE wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas ameendelea kuineemesha jumiya ya umoja wa wanawake mkoa wa Iringa (UWT) kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni nne (4,000,000) kwa jumuiya hiyo wilaya ya Iringa Mjini kwa ajili ya kuendeleza miradi ya umoja huo na kuondokana kuwa tegemezi.
 
Pesa hizo zimetolewa wakati wa baraza la umoja wa wanawake wilaya ya Iringa Mjini mkoani (UWT) lilofanyika katika ukumbi wa chama cha mapinduzi ulipo Iringa Mjini na kuhudhuriwa na wageni wengi wakiwepo wabunge wa viti maalum ambao ni Ritta Kabati na Rose Tweve

Akizungumza katika baraza hilo MNEC Asas alisema kuwa amependezwa na mikakati ambayo imefanya na umoja huo wa wilaya ya Iringa Mjini kwa kuwa wanafanya kazi na viongozi pamoja na wananchi wa chini hivyo inakuwa rahisi kuendelea kukijenga chama hicho.

Nimeona kwenye hotuba yenu mmesema kuwa “mtahakikisha kuwa wanawake wanajiunga kwenye vikundi vya uzalishaji kama vile vikoba ,saccos na vikundi vingine ili waweze kupata mafunzo stahiki ya ujasiliamali kwa lengo la kupambana na hali ya kiuchumi na kuongeza kipato,”hakika kwa kufanya hivi mtawaokoa wanawake wengi sana kiuchumi. Alisema Asas 

Asas alisema kuwa nimesikia mnataka kuanzisha duka kwa ajili ya kuongeza ajira na kuongeza uchumi wa umoja huu,hilo ni jambo bora hivyo kwa kuona mikakati hiyo nawachangia kiasi cha shilingi milioni nne (4,000,000) ili wafikie malengo ya kujiendesha na kuacha kuwa tegemezi.

Aidha Asas alimpongeza mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Rose Twelve kwa jitihada alizozifanya za kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kutoa mitaji kwenye kata kumi na saba  kwa kutoa kiasi cha shilingi laki sita kwa kila kata,hivyo kwa kuliona hilo MNEC alisema kuwa atachangia kiasi cha shilingi laki tano kwa kila kata hivyo kwa kata zote 18 za wilaya ya Iringa Mjini atachangia kiasi cha shilingi milioni tisa (9,000,000).

Kwa hili sipepesi macho nampongeza sana mbunge Rose Tweve kwa kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha wanawake wanapata mafanikio kwa kuwawezesha kama alivyofanya kwa kufanya hivyo amefanikiwa kuwafikia wanawake walio na kipatao cha chini kabisa na nitaendelea kukusaidia mbunge kwa kazi unazozifanya kwa ajili ya maendeleo” alisema Asas

Kwa upande wake katibu wa UWT wilaya ya Iringa Mjini Frola Kapalia alimshikuru MNEC Salim Asas kwa kutoa msaada mkubwa kama huo ambao hata wao hawakutegemea kutokea kitu kama hicho,ambapo ukipiga mahesabu utagundua kuwa ametoa jumla ya shilingi milioni kumi na tatu(13,000,000) kwa UWT Iringa Mjini

“Ametoa shilingi mioni nne kwa UWT na ametoa milioni tisa (9,000,000) kwa ajili ya kuongezea nguvu kwenye mfuko wa mbunge Rose Tweve hivyo lazima tujivunie kuwa na MNEC wa namna hii” alisema Kapalia

0 comments