Tuesday, 13 March 2018

Naibu waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara katika Kitongoji cha Mahiga, Kijiji na Kata ya Mwakitoliyo, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kusikiliza kero za wananchi hao, Juzi 11 Machi 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Wakazi wa Kitongoji cha Mahiga, Kijiji na Kata ya Mwakitoliyo, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakimsikiliza Naibu waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb) wakati wa mkutano wa hadhara, Juzi 11 Machi 2018.
Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe Ahmed Salum akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo kabla ya kumaribisha Naibu waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb) kusikiliza kero za wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika Kitongoji cha Mahiga, Kijiji na Kata ya Mwakitoliyo, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Juzi 11 Machi 2018.
Naibu waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb) akiwatuliza wananchi wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika Kitongoji cha Mahiga, Kijiji na Kata ya Mwakitoliyo, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ili kusikiliza mgogoro baina ya wananchi hao na kampuni ya Henan Afro-Asia Geo Engineering co ltd kutoka nchini China, Juzi 11 Machi 2018
Naibu waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb) (Kushoto) akisikiliza malalamiko kwa baadhi ya Wakazi wa Kitongoji cha Mahiga, Kijiji na Kata ya Mwakitoliyo, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kabla ya mkutano wa hadhara uliofanyika Juzi 11 Machi 2018.

Na Mathias Canal, Shinyanga

Serikali imekiri kuwepo kwa changamoto katika ulipaji wa fidia kwa wananchi waliofanyiwa uthamini katika maeneo yao ili kupisha mradi wa uchimbaji wa madini ya dhahabu kupitia kampuni ya Henan Afro-Asia Geo Engineering co ltd kutoka nchini China.

Akizungumza Juzi 11 Machi 2018 na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara katika Kitongoji cha Mahiga, Kijiji na Kata ya Mwakitoliyo, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Naibu Waziri wa wizara ya madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb) amekiri kuwa zipo changamoto katika jambo hilo hivyo serikali itapitia upya tathimini sambamba na ulipaji wa fidia ili kuhuisha sintofahamu hiyo iliyopelekea wananchi hao kupaza sauti zao za malalamiko.

Mhe Biteko alisema kuwa katika sekta ya madini mnufaika wa kwanza lazima awe mtanzania kwani sheria ya madini ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2017 inaelekeza kuwa na uchumi fungamanishi kwa wananchi ili kuinua pato la wananchi sambamba na mchango wa sekta ya madini kwenye Pato la Taifa.

Aidha, Mhe Biteko aliwasihi wananchi hao kuwa watulivu katika kipindi kifupi ambacho serikali inapitia upya tathmini hiyo huku akiwasihi kuacha uvamizi katika eneo hilo kwani kufanya hivyo ni uvunjifu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi.

“Ndugu zangu wananchi Sio kweli kwamba wawekezaji ni wabaya lakini wanapaswa kutambua tu wakija kuwekeza nchini wanapaswa kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi ikiwa ni pamoja na kuwa na mahusiano mazuri na wananchi wanaoishi karibu na mradi huo” Alikaririwa Biteko (Mb)

Machi 10, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wananchi katika eneo la Nyasubi katika Halmashauri ya mji wa Kahama Mkoa wa Shinyanga wakati wa dhifa ya uzinduzi wa barabara ya Isaka-Ushirombo yenye urefu wa Kilomita 132, alimuagiza Naibu Waziri wa wizara ya madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb) kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe Ahmed Salum kufanya ziara na kuwasikiliza wananchi kuhusu malalamiko hayo ili serikali kutafuta ufumbuzi wa haraka.

Wananchi hao wanalalamikia kufanyiwa tathmini tofauti na matakwa ya sheria huku wakipatiwa malipo kiduchu pasina kufanyika mkutano wa hadhara wa maridhiano baina ya wananchi na muwekezaji huhu wakiomba kufanyika upya tathmini ya maeneo yao.

MWISHO
 Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas akiongea na wajumbe wa baraza la UWT manispaa ya Iringa lilofanyika katika ukumbi wa CCM sabasaba na kutoa jumla ya shilingi milioni
kumi na tatu(13,000,000) kwa UWT Iringa Mjini
 Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas akipokea zawadi kutoka kwa viongozi wa UWT manispaa ya Iringa
 Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas akibadilisha mawazo na mwenyekiti wa UWT manispaa ya Iringa Ashura Jongo pamoja na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

MJUMBE wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas ameendelea kuineemesha jumiya ya umoja wa wanawake mkoa wa Iringa (UWT) kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni nne (4,000,000) kwa jumuiya hiyo wilaya ya Iringa Mjini kwa ajili ya kuendeleza miradi ya umoja huo na kuondokana kuwa tegemezi.
 
Pesa hizo zimetolewa wakati wa baraza la umoja wa wanawake wilaya ya Iringa Mjini mkoani (UWT) lilofanyika katika ukumbi wa chama cha mapinduzi ulipo Iringa Mjini na kuhudhuriwa na wageni wengi wakiwepo wabunge wa viti maalum ambao ni Ritta Kabati na Rose Tweve

Akizungumza katika baraza hilo MNEC Asas alisema kuwa amependezwa na mikakati ambayo imefanya na umoja huo wa wilaya ya Iringa Mjini kwa kuwa wanafanya kazi na viongozi pamoja na wananchi wa chini hivyo inakuwa rahisi kuendelea kukijenga chama hicho.

Nimeona kwenye hotuba yenu mmesema kuwa “mtahakikisha kuwa wanawake wanajiunga kwenye vikundi vya uzalishaji kama vile vikoba ,saccos na vikundi vingine ili waweze kupata mafunzo stahiki ya ujasiliamali kwa lengo la kupambana na hali ya kiuchumi na kuongeza kipato,”hakika kwa kufanya hivi mtawaokoa wanawake wengi sana kiuchumi. Alisema Asas 

Asas alisema kuwa nimesikia mnataka kuanzisha duka kwa ajili ya kuongeza ajira na kuongeza uchumi wa umoja huu,hilo ni jambo bora hivyo kwa kuona mikakati hiyo nawachangia kiasi cha shilingi milioni nne (4,000,000) ili wafikie malengo ya kujiendesha na kuacha kuwa tegemezi.

Aidha Asas alimpongeza mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Rose Twelve kwa jitihada alizozifanya za kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kutoa mitaji kwenye kata kumi na saba  kwa kutoa kiasi cha shilingi laki sita kwa kila kata,hivyo kwa kuliona hilo MNEC alisema kuwa atachangia kiasi cha shilingi laki tano kwa kila kata hivyo kwa kata zote 18 za wilaya ya Iringa Mjini atachangia kiasi cha shilingi milioni tisa (9,000,000).

Kwa hili sipepesi macho nampongeza sana mbunge Rose Tweve kwa kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha wanawake wanapata mafanikio kwa kuwawezesha kama alivyofanya kwa kufanya hivyo amefanikiwa kuwafikia wanawake walio na kipatao cha chini kabisa na nitaendelea kukusaidia mbunge kwa kazi unazozifanya kwa ajili ya maendeleo” alisema Asas

Kwa upande wake katibu wa UWT wilaya ya Iringa Mjini Frola Kapalia alimshikuru MNEC Salim Asas kwa kutoa msaada mkubwa kama huo ambao hata wao hawakutegemea kutokea kitu kama hicho,ambapo ukipiga mahesabu utagundua kuwa ametoa jumla ya shilingi milioni kumi na tatu(13,000,000) kwa UWT Iringa Mjini

“Ametoa shilingi mioni nne kwa UWT na ametoa milioni tisa (9,000,000) kwa ajili ya kuongezea nguvu kwenye mfuko wa mbunge Rose Tweve hivyo lazima tujivunie kuwa na MNEC wa namna hii” alisema Kapalia

Monday, 12 March 2018

  Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akiongea na viongozi wa chama cha mapinduzi jimbo hilo walipokutaka mjini mafinga kuzungumzia changamoto za jimbo hilo na nini kifanyike kutatua changamoto hizo
  Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akiwa na viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi 

Na Fredy Mgunda,Iringa.

 MBUNGE wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi amesema kuwa vijiji vyote vya jimbo hilo vitapatiwa umeme wa LEA ambao unafadhiliwa na serikali kwa lengo la kuchochea maendeleo ya wananchi waliopo vijijini

Chumi amewatoa hofu hiyo wananchi wa jimbo hilo juu ya upatikanaji wa umeme wa LEA wakati alipofanya mkutano na viongozi wa chama cha mapinduzi wa kata zote wa jimbo hilo.

Lakini mbunge huyo alitoa dira ya muelekeo wa jimbo hilo kimaendeleo kwa kuwakumbusha wapi walikotoka na wapi wanaendelea

Saturday, 10 March 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa uzinduzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga yenye urefu wa kilomita 45, Leo Jumamosi 10 Machi 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akikata utepe ishara ya uzindua wa barabara ya Uyovu-Bwanga yenye urefu wa kilomita 45, Leo Jumamosi 10 Machi 2018. 
Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akimshuku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa fedha zilizotolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa shule na vituo vya afya Wilayani bukombe wakati wa dhifa ya uzinduzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga yenye urefu wa kilomita 45, Leo Jumamosi 10 Machi 2018.
Mamia ya wananchi Wilayani Bukombe Mkoa wa Geita wakimlaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kuzindua barabara ya Uyovu-Bwanga yenye urefu wa kilomita 45, Leo Jumamosi 10 Machi 2018. 

Na Mathias Canal, Ushirombo-Geita

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli Leo Jumamosi 10 Machi 2018 amezindua rasmi barabara ya Uyovu-Bwanga yenye urefu wa kilomita 45 ambayo imekamilika kwa kujengwa kwa kiwango cha lami.

Katika dhifa hiyo iliyofanyika katika Kijiji cha Runzewe Kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita, Rais Magufuli amesema kuwa Tanzania ni nchi ya tano kwa ukuaji wa uchumi barani Afrika hivyo wananchi wanapaswa kuwapuuza wanasiasa wanaohubiri kuporomoka kwa uchumi kwa matakwa ya kujiimarisha kisiasa.

Alisema katika kipindi cha miaka miwili serikali imefanya kazi kubwa ikiwa ni pamoja na kuimarisha sekta mbalimbali kwa usimamizi nzuri katika rasiliamali Madini, kuboresha sekta ya elimu ambapo wanafunzi wanasoma bure kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari.

Alisema kuwa, bajeti ya mwaka 2015 katika sekta ya afya ilikuwa ni Bilioni 31 lakini serikali kwa kutambua umuhimu wa kuimarisha afya za watanzania ambapo sasa bajeti imefikia shilingi Bilioni 239 na hayo ni matokeo ya umoja na amani iliyopo nchini.

Rais Magufuli amesema amani iliyopo nchini Tanzania imejengwa chini ya uasisi wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ikasimamiwa vyema na marais wastaafu Mhe Ally Hassan Mwinyi, Mhe Benjamin Mkapa pamoja na Mhe Jakaya Mrisho Kikwete.

"Mambo yanayofanywa na serikali hayawezi kuyafurahisha mataifa mengine hivyo mataifa hayo yanawatumia watanzania wenyewe kutengeneza chuki dhidi ya serikali yao" Alikaririwa Rais Magufuli

Aliongeza kuwa kukamilika kwa barabara hiyo imekuwa sehemu ya Kuchochea shughuli za maendeleo ya kijamii katika usafirishaji wa mazao, kurahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa, sambamba na kuongeza pato la Mkoa wa Geita na Taifa kwa ujumla.

Katika hatua nyingine Rais Magufulu amewasihi wananchi Kutovamia hifadhi za Taifa badala yake kuwa wavumilivu na kuiacha serikali ifanye, kwani watatumwa wataalamu wa Wizara ya ardhi na maliasili ili kuratibu na kuona namna ya kuyagawa maeneo kwa ajili ya wafugaji na wakulima.