Saturday, 16 March 2013

DIAMOND ATAKA AKUMBUKWE KUPITIA MSIKITI

Mwanamuziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul anaetamba kwa jina la Diamond Platinum ametangaza nia ya kujenga msikiti ili mashabiki wamkumbuke kupitia msikiti huo.

Diamond akizungumza jana alisema kuwa yuko katika mchakato wa kutafuta eneo la kujenga msikiti ikiwa ni namna ya kurejesha shukrani kwa mashabiki wake, na kupitia msikiti huo utatoa taswira nzuri ya muziki wa kizazi kipya.

Diamond aliongeza kuwa ana amini mashabiki wake watamkumbuka kupitia msikiti huo pale atakapo ingizwa katika tumbo la ardhi na Mwenyezi Mungu atamtilia wepesi katika kazi zake.

"Hata mimi ni kifa leo na keshokutwa, mashabiki wangu wawe wananikumbuka kwa hili (kujenga msikiti), naamini kufanya hivi hata Mwenyezi mungu atazidi kuniwezesha kwa hili." alisema Diamond.

--
MSUNI COMPUTER SOLUTION
TUNATATUA TATIZO LA COMPUTER YAKO
065 718 4421
065 714 8283 (habib)
www.aboodmsuni21.blogspot.com

0 comments