Sunday, 23 June 2013

HUKUMU YA KUFANYA SHEREHE USIKU WA TAREHE KUMI NA NNE KUAMIA KUMI NA TANO YA MWEZI WA SHAABANI ,PAMOJA NA FUNGATAREHE 15 YA MWEZI WA SAHAABANI

Na  MIMI NI MUISLAMU

HUKUMU YA KUFANYA SHEREHE USIKU WA TAREHE KUMI NA NNE KUAMIA KUMI NA TANO YA MWEZI WA SHAABANI ,PAMOJA NA FUNGATAREHE 15 YA MWEZI WA SAHAABANI:


Alikuwa mtume swala Allahu alayhi wasallam akifunga mwezi wa Shaabani wote isipokuwa siku chache tu.Kama ilivyo pokelewa toka katika hadithi sahihi.


Ni juu yetu kumuiga kipenzi chetu na kigezo chetu mtume wetu rehema na amani ziwe juu yake na kufuata nyayo zake.

Katika kuonesha fadhila za mwezi huu,imepokelewa ya kuwa ndani ya mwezi huu matendo ya waja huinuliwa kwa Mola wao,pia waja husamehewa madhambi yao isipokuwa wale walio kosana mpka watakapo fanya suluhu.

Wanawazuoni wakatofautiana kuhusiana na kufunga siku hii yaani tarehe 15 ya mwezi wa shaabani ambayo ni kesho:


Rai yenye nguvu katika mas ala hii ni kuwa,haifai kufunga siku hii wala kufanya sherehe mbai mbali zinazofanywa,vile vile kuikhusisha siku hii na kisimamo cha usiku na kuomba dua mbali mbali.Bali ni juu yetu kufunga na kutekeleza ibada mbali mbali kwa kuiga vile alivyokuwa akifanya mtume. Kwani hakuna hadithi sahihi kutoka kwa mtume inayo inayo zungumzia fadhila za kuikhusisha siku hii kwa kufanya ibada au sherehe.

Sheikh Ibun Jibrin aliulizwa:



Nimesoma katika baadhi ya vitabu ya kuwa funga siku ya kumi na tano ya mwezi wa Shaabani ni bidaa miongoni mwa bidaa.Nikasoma katika vitabu vingine wansema ya kuwa inapendeza kufunga tarehe kumi na tano ya mwezi wa shaabani.Ni ipi hukumu ya mwisho juu ya mas ala hii?

 Jibu:

Haijathibiti hadithi sahihi toka kwa mtume kuhusiana na fadhila za nusu ya shaabani ili ifanyiwe kazi...bali zimepokelewa baadhi ya athari toka kwa mataabiin,kauli ambazo hazinasibiswi kwa mtume,na kuna hadithi nyingine ni zakutengenezwa na nyingine ni dhaifu sana....kutokana na hivyo,haifai kusherehekea usiku wa kuamkia siku hiyo ya kumi na tano wala kufunga mchana wake,wala kuikhusisha na ibana maalumu.
WALLAHU A-ALAM

 Na sheikh Muhamad Swaleh Almunjid akasema:

Iwapo kama mtu ataamua kufanya ibada za usiku,usiku wa kuamkia siku hiyo- ya kumi na tano ya mwezi wa shaabani-kama anavyofanya katika usikuwa wa siku nyingine,pasina ya kuzisha ibada fulani wala kuongeza juhudi za ziada,basi hakuna tatizo. Vile vile iwapo kama mtu atafunga tarehe hiyo 15 kwa kuwa ni siku ya tatu miongoni mwa siku nyeupe{Ayyamul biidh},pamoja na kufunga kabla yake 14 na 13,au kwa kuwa tarehe 15 hiyo ya mwezi wa shaabani ni siku ya jumatatu au alkhamisi ,basi hakuna tatizo iwapo kama atafanya ibada hizo pasina ya kuitakidi fadhila za ziada juu ya siku hiyo. WALLAHU TAALA A-ALAM



0 comments