Tuesday, 2 July 2013

WAISLAMU KAZI KWENU, MUM WATANUA WIGO, SASA KUTOA CERTIFICATE NA DIPLOMA

Chuo cha waislam Morogoro kimeanzisha utoaji wa Diploma na Cetficate za fani mbalimbali, ambazo zinatarajiwa kuanza kutolewa katika mwaka wa masomo wa 2013./14 utakaoanza hapo baadae.

Kwa mujibu wa taarifa iliyo tufikia Tembezi Za Msuni na kudhibitishwa na mmoja wa waadhiri wa chuo hicho ustadh Said Jafu zinasema kuwa wanafunzi wenye principle moja 'E' katika matokeo ya Advance (kidato cha sita) wataoata fursa ya kusoma diploma miaka miwili na wale wenye D 4 katika matokeo ya kidato cha nne watasoma certificate

"Chuo kikuu Cha Waislam Morogoro kinakutangazien nafasi za masomo ya Diploma na Certificate: Dp/CT in journalism, sc and lab technology, islamic banking & finance,  procurement & logistics management,  law & shariah. and Ct in sign language and Arabic language," ilieleza taarifa tulio tumiwa.

"Sifa Dip: E moja ya A'leval. Ct: D 4 za  O'leval. Ada kwa Dip 800,000. Cet 700,000. Muda Dip miaka 2. Ct mwaka Moja. Fikisha ujumbe huu kwa unaowajua." ili hitimisha taarifa hiyo.

.

0 comments