Friday, 13 September 2013

WAKULIMA MVOMERO KLULIMDA MASHAMBA YAO

N a Joseph Malembeka

WAKULIMA wilayani Mvomero, Morogoro, wameanzisha vikundi vya ulinzi na operesheni dhidi ya wafugaji kulisha mifugo shambani.

Operesheni hiyo iliyoanza Septemba 9 imefanikiwa kukamata ng’ombe 700 katika kijiji cha Kisala, kata ya Sungaji, wakiwamo zaidi ya ng’ombe 1,200 waliolipiwa faini ya sh milioni 7 mbele ya mkuu wa wilaya hiyo, Anthony Mtaka, zilizolipwa papo hapo.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kisala, Shaban Abdallah, alisema lengo la operesheni hiyo ni kukomesha vitendo hivyo vinavyowatia hasara mara kwa mara; pia kuna sheria ndogo ya faini ya sh 50,000 kila ng’ombe atakayekamatwa shambani.

“Baada ya kukubaliana faini hiyo kwenye mkutano wa kijiji na kuungwa mkono na Mkuu wa Mkoa, Joel Bendera, ambaye alitupatia eneo la kuwahifadhi wanayama hao pindi wakikamatwa, wananchi waliamua kuwa na kikosi maalumu cha jadi kuwakabili hawa wafugaji na matunda ndio haya,” alisema ofisa mtendaji huyo.

Kwa mujibu wa mtendaji huyo hadi ng’ombe hao wanakamatwa zaidi ya ekari 50 zenye mazao mbalimbali yakiwemo mahindi, mpunga na miwa zinakisiwa zimeharibiwa na mifugo hiyo.

Awali mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho, Shija Msafiri, alisema wananchi wameamua kuwa na ulinzi wa jadi kupitia mafunzo maalumu ya ‘Ujaki’ kutoka Ukaguruni, baada ya kuona hakuna msaada kutoka serikalini hata wanapowakamata na kuwafikisha kwenye vyombo husika.

0 comments