Sunday, 1 September 2013

WAKULIMA WAWAZUIA WASAFIRI

Wakulima wa kijiji cha Doma mkoani Morogoro wameingia barabarani toka asubuhi na kuzuia njia inayo unganisha kijiji hicho cha Doma na mbuga za Mikumi.

Wakulima hao waliojazana kwenye daraja lililopo katika barabara hiyo inayounganisha mkoa wa Morogoro na mkoa wa Iringa na kupelekea wasafiri kukwama kwenye daraja hilo toka mida ya asubuhi mpaka tunapoandika taarifa hii hakuna gari lililo weza kukatisha darajani hapo.

Wakulima hao wanasema kuwa hawataki kumsikiliza mtu yoyote isipokuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro ili wapate kuelezea adhaa yao wanayo ipata toka kwa wafugaji.

Kwa mujibu wa moja ya wakulima aliyepaywa kuhoji na radio IMan FM a,ese,a kuwa wamechoshwa na vitendo wanao fanyiwa na wafugaji ikiwemo kupigwa na baadhi ya dugu zao hivi sasa wako hospitalini kutokana na kumizwa na wafugaji hao.

Mkulima mwingine alisema kuwa wamekuwa wakipeleka malalamiko yao serikalini bila kupata majibu ya aina yoyote ile na hivyo kuwapelekea kufunga barabara hiyo ili madai yao yapate kusikilizwa.

Wakati tukiwa tunaenda mitamboni mkuu wa polisi mkoa Morogo alikuwa anaelekea kwenye eneo la tukio, hilki kuangalia namna ya kuifungua barabara hiyo, na kuwa wezesha wasfii waliokwama kwa takribani masaa 4 waweze kuendelea na safari zao.

0 comments