Monday, 24 February 2014

BAVICHA: Matokeo kidato cha nne ni ya kisiasa

By    
BARAZA la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) limesema matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa na serikali juzi ni ya kisiasa zaidi.

Katibu Mkuu wa BAVICHA, Deogratias Munishi, alibainisha hayo jana na kuongeza kuwa serikali imejinasibu kuwa kiwango cha ufaulu kimepanda kwa asilimia 15.17 ukilinganisha na matokeo ya mwaka jana huku ikiwa yako kisiasa zaidi na yanashindwa kuakisi ukweli  wa  hali ya elimu nchini.

Alisema matokeo hayo yameendelea kuonyesha jinsi mfumo wa elimu nchini ulivyoharamu kwa vijana,  kwani  kundi la wanafunzi waliofanya mtihani huo ni wale waliomaliza darasa la saba mwaka 2009.

“Wanafunzi takribani 898,420 wameshatupwa nje ya mfumo kwa kati ya 2009 na 2013, kwani waliotarajiwa kumaliza darasa la saba 2009 walikuwa 1,024,488 huku 502,624 wakifeli vibaya, 493,333 wakidaiwa kufaulu na 28,531 wakiwa haijulikani wamepotelea wapi na hadi wanafunzi 404,083 waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2013 maana yake wanafunzi 89,250 walishapotelea njiani leo hii wanaleta siasa,” alieleza Munishi.

0 comments