![]() |
| Moses mwanamume anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja atafuta hifadhi nchini Marekani |
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametia saini mswada
wenye utata unaotoa adhabu kali kwa watakaopatikana wakishiriki mapenzi
ya jinsia moja.
Mswada huo ambao sasa utakuwa sheria, unatoa adhabu ya kifungo cha miaka 14 jela kwa wale watakaopatikana na hatia kwa mara ya kwanza,
Adhabu ya maisha jela itatolea kwa watu watakaopatikana na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja zaidi ya mara moja kati ya watu wawili waliokubaliana kufanya hivyo.
Adhabu hiyo pia itatolewa kwa wale wanaopatikana na hatia ya kuwahusisha watoto katika vitendo hivyo, walemavu au kumuambikiza mtu virusi vya Ukimwi.
Mswada huo umepigiwa debe sana nchini Uganda, lakini mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yameulaani.
CHANZO: BBC SWAHILI




0 comments