Sunday, 16 February 2014

NCHI YA MYANMAR NI JELA YA MATESO KWA WAISLAMU WA KABILA LA ROHINGYA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgfE7JLEkNgpNjpees8JVV4QYAlULlWRMOdU2DNq61wqEV92s0RGzjT2J-pYOYDnNlh4DwtisbFhDBZZaopQm-y0189iqQ7SNac0aPtVyPld0TViFVNKlcLC3NEtI4KcaBUI_7X7HRx2LOG/s1600/myn.jpg
Waislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar ambao wamekuwa wakishambuliwa na kuuawa kinyama na magaidi wa Kibudha wa nchi hiyo hawataki kurejea katika makazi yao wakihofia usalama wa maisha yao.

Kanali ya Televisheni ya al-Akhbar al-Aan imetangaza leo kuwa, nchi ya Myanmar imegeuka na kuwa jela kwa Waislamu walio wachache nchini humo na kwamba, Waislamu hao wamekuwa wakikosa huduma muhimu kama za afya na elimu huku serikali ya nchi hiyo ikikataa hata kuwapatia vitambulisho. 

Ripoti hiyo inabainisha kwamba, kutokana na kutokuwa na vitambulisho, Waislamu wa Rohingya wamekuwa wakilazimika kuondoka nchini humo kupitia njia zisizo halali. 

Waislamu wengi wa kabila la Rohingya wamekuwa wakikimbilia katika nchi jirani za Thailand na Bangladesh. 

Kinachosikitisha zaidi ni kwamba, asasi za kimataifa zimekuwa hazizishinikizi nchi jirani na Myanmar ili zisiwafukuze Waislamu hao kutoka katika nchi hizo, imebainisha ripoti hiyo.  

Tangu mwezi Juni mwaka 2012 magaidi wa Kibudha wamekuwa wakiwashambulia Waislamu wa kabila la Rohingya katika jimbo la Rakhine nchini Myanmar ambapo hadi sasa maelfu ya Waislamu wameuawa huku wengine zaidi ya laki mbili wakiachwa bila makao.

0 comments