Sunday, 16 February 2014

MTOTO WA BHUTO ATOA WITO WA KUKABILIANA NA TALIBAN


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg5_d0U60Zi2Eg1TJ9esZ-CPcpAjFi9_rB70DYPxril0l29CveqM533AVuUyZOs2TFsbRanR3R58G9DlWZ0Q6vCpfOQr75bzNff4n-W7LgrQb0YYK_tonsDY1az2Vmto5jNkhdJXsHbTzdo/s1600/bhuto.jpg

Mwana wa waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Bilawal Bhutto Zardari ametoa wito wa kukabiliana na harakati za wapiganaji wa Taliban wanaotaka kuzusha hofu na woga katika nchi hiyo.

Akihutubia katika jimbo la Kusini la Sindh hapo jana, Bilawal Bhutto aliwataka wananchi wa Pakistan kufanya jitihada za kukabiliana na wanamgambo wa kundi la Tehrik Taliban Pakistan (TTP) na kusema kuwa nchi hiyo haikubali sheria za kigaidi. 

Ameongeza kuwa, wananchi wa Pakistan wengi wao ni Waislamu na kwamba makundi ya kigaidi hayawezi kuwafundisha dini.

Benazir Bhuto aliuawa na kundi la Taliban la TTP katika shambulio la kigaidi mwaka 2007. Awali kundi hilo lilikuwa limetishia kumuua waziri mkuu huyo wa zamani wa Pakistan lakini lilikanusha kuhusika na mauaji hayo.

Serikali ya Pakistan hivi karibuni ilianza mazungumzo ya amani na kundi hilo linalopigana kwa miaka kadhaa katika eneo la kikabila la kaskazini magharini, lakini mazungumzo hayo yamekwama kutokana na kuweka masharti ya kutumika sheria ya kiislamu kwanza katika nchi ya Pakistan.

0 comments