
Moqtada al-Sadr akitoa taarifa kwa vyombo vya habari
Kiongozi wa Dhehebu la Shia nchini Iraq Moqtada al-Sadr ametoa taarifa akitangaza kujiuzulu kwake katika ulingo wa kisiasa.
katika
tangazo ambalo halikutarajiwa na wengi na ambalo liliwekwa katika
mtandao wake,Bwana Sadr amesema kuwa hatashikilia wadhfa wowote wa
serikali wala kuwa na wawakilishi bungeni.
Taarifa hiyo pia imesema kuwa atazifunga afisi zake zote isipokuwa zile za kutoa misaada pekee.
Bwana Sadr na wanamgambo wake wa Mahdi walipata ushawishi nchini Iraq baada ya uvamizi wa marekani nchini humo mnamo mwaka 2003.
lakini
katika miaka ya hivi karibuni amepoteza umaarufu wake kufuatia mzozo
kati yake na waziri mkuu nchini humo Nouri al-Maliki.
Wakati huohuo
Aliyekuwa makamu wa rais nchini Iraq amemlaumu waziri mkuu Nouri Al
Maliki kwa kusababisha ghasia kati ya wanamgambo wa dhehebu la sunni na
vikosi vya serikali ambavyo vinaushikilia mkoa wa Anbar tangu mwezi
Disemba.
katika
mahojiano na BBC,Tariq al-Hashemi ameishtumu serikali hiyo inayoongozwa
na watu wa dhehebu la shia kwa kuzua mgongano huo, kupitia kuwabagua
watu wa dhehebu la sunni mbali na kupuuzilia mbali maandamano ya amani.
Bwana
Hashemi kwa sasa anaishi kama mkimbizi nchini Uturuki baada ya mahakama
moja nchini humo kumpatia hukumu ya kunyongwa kwa madai ya kuendesha
magenge ya uhalifu,mashtaka anayoyapinga.
Bwana
Hashemi anasema kuwa madai ya serikali ya Iraq kwamba uasi huo
unaongozwa na vikosi vinavyoshirikiana na kundi la Alqaeda ni njama ya
kutotaka kuwajibika mbali na kuvutia hisani kutoka kwa jamii ya
kimataifa.



0 comments