
Mohammed Morsi akiwa mahakamani
Aliyekuwa
rais wa Misri Mohammed Morsi atafika katika mahakama moja mjini Cairo
ili kusikiza mashtaka ya upelelezi na njama ya kutaka kutenda ugaidi
yanayomkabili.
Bwana Morsi aling'atuliwa mamlakani na jeshi mnamo mwezi Julai na sasa anakabiliwa na mashtaka mengine matatu.
katika
kesi hiyo yeye na wanachama wengine 35 wa vunguvu la Muslim Brotherhood
wanatuhumiwa kwa kushirikiana na makundi ya kigeni kama vile
Hamas,Walinzi wa mapinduzi nchini Iran na Hezbollah kupanga mashambulizi
nchini Misri.
Iwapo atapatikana na hatia bwana Morsi anakabiliwa na hukumu ya kifo.



0 comments