Monday, 17 February 2014

SHULE ZA NEW YORK, MAREKANI KUWA NA MAPUMZIKO SIKUKUU ZA EID AL-FITR NA EID AL-ADHA

By    
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjkrqf-tFwMZlcxHpWzWhBZ4Nkz0DBBsc8o8nyiEMGcW-yYxwFmZXDqLJ2ULNFc8mh0RPYnTSaz9_Cs6Gd0L-pEZ31ajowE6Y_O1gR3nJhVs4hTa2ptGreClvTdajOXx_RurWOolJlULtoN/s1600/nyc-schools.jpg
Meya wa jiji la New York City Bill de Blasio ametangaza mipango ya kutekeleza sera ya kuwa na mapumziko kwa shule za umma za jiji hilo wakati wa sikukuu za kiislamu za Eid al-Fitr and Eid al-Adha.

Wakati wa kampeni za uchaguzi mwezi Oktoba, Meya alitangaza ahadi yake kwamba atazitambua sikukuu za kiislamu za Eid al- Fitr na Eid al- Adha.

 "Asili ya taifa hili ni la watu wa dini mbalimbali waliokuwa pamoja, hivyo ndiyo sababu tunaheshimu imani za waislamu kwa kutoa likizo ya Eid kwa ajili ya watoto katika mfumo wetu wa shule," alisema de Blasio.

Kwa Hatua hiyo Baraza la kiislamu la Marekani la jiji la New York the Council on American-Islamic Relations (CAIR-NY) limempongeza Meya kwa mpango huo wa kufunga shule wakati wa sikukuu za kiislamu.

Mjumbe wa Bodi ya Baraza hilo Zead Ramadhan alisema ni jambo la kufurahisha kwa jiji la New York kutambua umuhimu wa wanafunzi wa kiislamu kuwa na haki ya kupumzika katika siku za sikukuu ya dini yao. 

kabla ya Hatua hii Zead Ramadhan anasema iliwafanya wanafunzi kuwa njia panda na kulazimika kukosa masomo yao kwa kuheshimu na kuadhimisha imani yao. Alisema jambo hili liliwafanya kukosa haki ya masomo. 

"Tunampongeza Meya De Blasio kwa hatua yake hii muhimu ya kutambua haki za watu wa dini nyingine"

0 comments