Wednesday, 19 February 2014

SHIRIKA LA KUZUIA UKIMWI DUNIANI UNAIDS LATAKA UGANDA KUTUPILIA MBALI SHERIA DHIDI YA MASHOGA.

Shirika la kuzuia la Umoja wa Mataifa linaloongoza harakati dhidi ya Ukimwi, UNAIDS nalo limepaza sauti dhidi ya muswada wa sheria wa kupinga mapenzi ya jinsia moja nchini Uganda likisema ukiwa sheria utasababisha ongezeko la maambukizi ya virusi vya Ukimwi na kinyume na haki za binadamu.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Michel Sidibé amesema Uganda ilikuwa nchi ya kwanza ya kiafrika kuvunja mipaka na kujumuisha makundi ya pembezoni katika kukabiliana na ukimwi lakini sheria hiyo sasa itatumbukiza kapuni mafanikio yote yaliyopatikana.

Ameitaka serikali ya Uganda kutupilia mbali muswada huo akieleza kuwa utakuwa na madhara kwenye afya ya kijamii kwani utafiti umeonyesha kuwa mashoga wanapobaguliwa, wanakuwa na hofu kusaka huduma za kinga au tiba dhidi ya Ukimwi.


Chanzo:Ahbaabur

0 comments