Monday, 24 February 2014

WAISLAMU WAPENDEKEZA ADHABU YA KIFO KWA MASHOGA NCHINI MALAWI

By    
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhcuAsxrhT9mMS_eFwmk80wYSxwlmCZheM3obeLfya8o_hn8RnsDFe_RM6ZoMP0gkub4BSbREHox6YJn2e_GAnx_-R49-OXKYRY0JHGIiFTpcbLH1__1tglYutAySjPJRU0_hrDhC1cpGoc/s280/malawi.jpg
 



Jumuiya ya waislamu ya nchini Malawi imetoa wito kwa serikali ya nchi hiyo kuweka sheria ya adhabu ya kifo kwa yeyote atayebainika kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Pendeko hilo limekuja wakati baadhi ya mashirika na taasisi za kijamii zikiishinikiza serikali ya nchi hiyo kuondoa adhabu ilipo sasa.

Nchini Malawi adhabu ya mtu atakeyejihusisha na mahusiano ya jinsia moja ni kifungo cha miaka 14 jela.

Akizungumza kwa niaba ya waislamu wa Malawi katibu mkuu wa jumuiya ya Waislamu Dk Salmin Omar Idris alisema sheria iliyopo bado haijasaidia kuondosha tatizo bali kuweka sheria ya kifo kwa kila atakayebainika kujihusisha na Ushoga.

"japokuwa malawi inaonekana kama ni nchi ya kawaida iliyobarikiwa na Mwenyezi Mungu lakini tunawaogopea raia wenzetu ambao hawamuogopi Mungu kwa kufanya matendo ya kumchukiza", alisema Dk Salmin.

"Hata wanyama kama mbuzi hawawezi kufanya mahusiano ya jinsia moja kwa nini tufanye sisi wanadamu ambao mwenyezi Mungu ametupa kheri nyingi pamoja hekima?, alihoji Dk Salmin.

Alisema kwamba kunahitajika kuwa na adhabu ya kifo ili kuondosha tatizo hilo kwani adhabu hiyo ndio njia pekee ya kuondoa jamii ya mashoga.

Shirika la Umoja wa mataifa la kuzuia Ukimwi Duniani pamoja na taasisi ya sheria na haki za binadamu ya malawi wemeomba kubadilishwa sheria ya sasa kwa madai ipo kinyume na haki za binadamu.

Mwaka 2011 mahakama moja ya mji wa Blantyre iliwahukumu watu watatu kwenda jela miaka 14 kwa kosa la kujihusisha mahusiano ya jinsia moja.

0 comments