
Waasi wa Kikristo wa Anti Balaka katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wamesema kuwa hawatakubali kuweka chini silaha zao eti hadi pale waasi wa Seleka ambao ni Waislamu nao pia watakapoweka silaha zao chini.
Kiongozi wa kundi hilo Sebastien Wenezoui amesema, wataweka silaha zao chini mbele ya jamii ya kimataifa iwapo pia waasi wa Seleka watapokonywa kwanza silaha.
Hata hivyo taarifa zinasema kuwa, waasi wa Seleka wametawanyika na hivi sasa wanamgambo wa Kikristo ndio tishio la amani na utulivu wa nchi hiyo.
Ripoti zinasema kuwa magenge ya Wakristo wenye misimamo mikali kutoka kundi la Anti-Balaka wamewaua maelfu ya Waislamu katika nchi hiyo huku mamia ya maelfu wakilazimika kukimbilia katika nchi jirani.
Wakati huo huo, mauaji dhidi ya Waislamu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati bado yanashuhudiwa ambapo juzi Waislamu watatu walishambuliwa kwa kupigwa risasi na watu waliokuwa ndani ya gari na kuuawa.
Taarifa zinasema kuwa, baada ya kuwaua Waislamu hao watu hao walianza kutoa nara dhidi ya Waislamu.



0 comments