Monday, 24 February 2014

ASKOFU TUTU ATETEA USHOGA, AMTAKA MUSEVENI ASISAINI MUSWADA WA SHERIA YA KUPIGA MARUFUKU USHOGA

By    

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEigrnk6hzGNpc_VPvvFC61Tlks0GMv7v01w-psBrzBGjVmCwEqifNxXrgfxTAb9ThB6Jo1GwJE0OB8VCMeSzetdgKPDxXwfANbny5wYrR5hf5xen1pQZ5pygrytDy0kvkOYeWgcXZiqSnPJ/s280/Desmond-Tutu-011.jpg
 


Askofu mstaafu wa Cape Town, Desmond  Mpilo Tutu, amemsihi Rais Museveni wa Uganda asitie saini mswada ulioleta utatanishi kuhusu wapenzi wa jinsia moja.

Askofu Tutu wa kanisa la kianglikana, aliyewahi kupata tuzo ya amani ya Nobel, alisema amevunjika moyo kuwa Rais Yoweri Museveni anaonesha kubadilisha msimamo wake, kwa vile awali alisema kuwa hataruhusu mswada huo kuwa sheria.

Desmond Tutu alisema haistahiki kuwa na ubaguzi kama huo, na alitoa mifano ya mfumo wa zamani wa ubaguzi wa rangi uliokuwako Afrika Kusini na ubaguzi wa Wa-Nazi wa Ujerumani.

Alisema hiyo ni mifano mibaya kabisa. Awali mswada wa Uganda ulipendekeza kifo kwa vitendo vya kulawiti na baadae kubadilishwa kuwa adhabu ya kifungo cha maisha.

0 comments