
HALMASHAURI ya Jiji la Arusha, imebomoa nyumba zake kwenye maeneo ya Kilombero, Themi na Kaloleni ambazo zilikuwa zinakaliwa na wapangaji 216.
Hatua hiyo imepokewa kwa hisia tofauti miongoni mwa madiwani na wapangaji hao ambao walikuwa wakipinga utekelezaji wa hatua hiyo kwa madai kuwa zoezi hilo halizingatii utu wa watu.
Kazi ya kubomoa nyumba hizo iliyofanyika kwa kutumia tingatinga, lilianza jana majira ya saa tisa alfajiri chini ya ulinzi mkali wa askari wa kutuliza ghasia (FFU) wakiwa na silaha pamoja na mgambo wa jiji.
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, akizungumza na Tanzania Daima jana, alisema hata kama kuna umuhimu wa kuwaondoa wananchi hao, ni vema zoezi hilo likafanyika kiungwana kwa kuwaongezea muda ili waweze kutafuta mahali pa kuhamia.
CHANZO: TANZANIA DAIMA



0 comments