Picha ya polisi wa Saudi Arabia akiwa amekanyaga na kiatu kwenye eneo Tukufu la Kaaba.
Kitendo cha askari huyo kukanyaga kwa kiatu eneo tukufu la kaaba limezua sokomoko kwenye vyombo vya habari katika ulimwengu wa Kiislamu.
Gavana wa mji wa Makkah, Mwanamfalme Mishal Bin Abdullah Bin Abdul Aziz, ameamuru uchunguzi
ufanyike juu ya tukio hilo, akisema kuwa kitendo hicho hakiwezi kuvumiliwa.
Aidha Mwanamfalme Mishal ametaka hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya polisi huyo kwa kushindwa kutambua heshima aliyopewa ya kutoa huduma katika eneo hilo tukufu zaidi kwa waumini wa dini ya Kiislamu duniani.
Katika tamaduni za Waarabu ni tusi kubwa kumuonesha mtu kikanyagio cha kiatu au kumtupia kiatu au kukikanyaga kitu kitukufu au mtu ukiwa hujavua kiatu.
Kaaba, ambayo ipo katika msikiti mtukufu wa Makkah ndio eneo takatifu zaidi kwa waislamu.



0 comments