![]() |
| Msuni |
Msuni ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa mwisho diploma katika chuo cha Al-Maktoum College Of Engineering and Technology akichukuwa fani ya Information tchnology, kesho anataraji kuwa miongoni mwa watakao vaa jezi za wanafunzi wa kitengo chake mwaka wa mwisho watakapo cheza na ndugu zao wa Electrical.
Timu ya wanafunzi wa mwaka wa mwisho diploma wanaochukuwa Information Techonology toka Al-Maktoum College of Engineering (Java FC) watachuana vikali na ndugu zao wa mwaka wa mwisho diploma wanao chukuwa Electrical (High Voltage FC), mchezo utakaochezwa saa nne na nusu asubuhi katika uwanja wa shule ya msingi ya Mbezi beach.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa wanafunzi wa Al-maktoum kucheza mechi ya wenyewe kwa wenyewe, ikiwa timu ya chuo teayari imeshawahi kushiriki mashindano matatu na kufanikiwa kutwaa ubingwa mashindano mawili kati ya matatu waliyopata kushiriki.
![]() |
| Baadhi ya Wachezaji wa Java FC wakiwa katika picha ya pamoja |
![]() |
| Abdallah H.I Sulayman (Abood Msuni) |







0 comments