Mabingwa mara tano wa kombe la dunia Brazil leo wamefunguwa michuano
hiyo ya kombe la dunia inayofanyika nchini Brazil kwa ushindi wa goli
3-1.
Brazil leo walikuwa na kibarua toka kwa Crotia, ambao katika mchezo wa
leo walianza kwa kukaa nyuma.
Crotia walikuwa wa mwanzo kupata goli katika dakika ya 10 beki Malcelo
akijifunga katika harakati ya kuokoa.
Kuingia kwa goli hilo kuliwafanya wa crotia kuzidi kujihami na
kuwaachia Brazil utawala wa mchezo ambapo Neymar aliisawazishia Brazil
na kupelekea mchezo kwenda mapumziko zikiwa sare ya 1-1.
Kipindi cha pili Crotia waliamua kufunguka na kupelekea timu
kushambuliana kwa zamu kabla ya Neymar kuifungia goli la pili Brazil
kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 70.
Kuingia kwa goli hilo liliwazidisha kasi Crotia na katika dakika ya 89
ama nusura wapate goli la kusawazisha.
Baada ya kukosa goli crotia walijikuta wanakubali kufungwa goli la 3
lililofungwa na Oscar na kupelekea mchezo kumaliza kwa brazil kushinda
goli 3-1.



0 comments