Friday, 13 June 2014

HARAMBE STAA KWENDA BRAZIL

By    
Mabingwa wa kombe la CECAFA Chalenge, Kenya (Harambe stars)
wanatarajia kuelekea Brazil kushuhudia mechi za kombe la dunia
lililoanza jana.

Harambe stars itapelekwa Brazil na raisi wa Kenya Uhuru Kenyata na
mkewe sambamba na kampuni ya bia ya Afrika mashariki, ambapo Kenyata
na mkewe watatoa dola 120,000 wakati kampuni ya bia itatoa doa 40,000.

Safari hiyo kwa wachezaji hao wanaunda kikosi hicho inatokana na ahadi
iliyotolewa na raisi Kenyata pamoja na mkewe wakati wa michuano ya
CECAFA, ambapo alisema endapo Harambe stars wangebakisha kombe nchini
Kenya, atawapeleka Brazil.

Raisi Kenyata alisema kuwa atawapeleka Brazil ili wakahamisike na
wawe na hamu ya kushiriki michuano hiyo mikubwa ya dunia kwa ngazi ya
mataifa.

Nae nahodha wa harambe stars Jeremy Onyago amesema kuwa "ni kama ndoto
kuwa kweli".

Bado haijafahamika harambe staz watakaa huko brazil kwa muda gani.

0 comments