Saturday, 14 June 2014

HISPANIA WAPIGWA MKONO, CAMEROON WAKIANZA VIBAYA

By    
Mabingwa watetezi wa kombe la dunia Hispania (Span) wameanza michuano
hiyo kwa aibu baada ya kubali kufungwa goli 5-1 na Uholanzi mchezo
uliomalizika hivi punde.

Katika mchezo huo hispania walikuwa wa mwanzo kupata goli kwa mkwaju
wa penati uliopigwa na Xabi Alonso baada ya Diego Costa kuchezewa
faulo kwenye eneo la hatari.

Uholanzi walisawazisha goli hilo kupitia kwa Roben Van persie na
kupelekea timu ziende mapumziko wakiwa sare ya goli 1-1.

Kipindi cha pili kilikuwa ni cha zaama kwa hispania ambapo zaama hilo
lilikuwa linaongozwa na Arjen Roben aliyeiandikia goli la pili
Uholanzi na goli la tano.

Goli la nne lilifungwa na Roben Van persie na kupelekea mchezo huo
kwisha kwa uholanzi kushinda goli tano dhidi ya moja la hispania.


Katika mchezo wa awali Cameroun wamekubali kufungwa goli 1-0 na Mexico.

0 comments