Saturday, 14 June 2014

COLOMBIA WAIDHIBU GREECE

By    
Timu ya taifa ya Colombia leo imeidhibu Greece goli 3-0 katika mchezo
wa kwanza wa siku ya tatu ya kombe la dunia nchini Brazil.

Colombia walianza kuandika goli katika dakika ya 5 kupitia kwa Pablo
Armero na kupelekea mchezo kwenda mapumziko Colombia wakiwa mbele kwa
goli 1-0.

Colombia waliandika goli la pili katika dakika 58 kupitia kwa Teofilo
Gutierrez, na goli la tatu likifungwa na James Rodriguez katika dakika
ya 90.

Mchezo mwingine wa kundi D kati ya Ivory coast na Japan utaanza saa
kumi usiku huku michezo ya kundi c ikichezwa saa nne na saa saba
ambapo Uruguay dhidi ya Coastarica na Uingeleza dhidi ya Italia.

0 comments