Sunday, 15 June 2014

UINGELEZA, URUGUAY WACHAPWA.

By    
Ungeleza na Uruguay wamejikuta wakianza vibaya michuano ya kombe la
dunia baada ya kuchezea kichapo toka kwa Italy na Costarica.

Costarica wakitokea nyuma wameichapa Uruguay goli 3-1, magoli ya
kifungwa na Joel Campbel katika dakika ya 54, Oscar Duarte dakika ya
57 na Marco Urema katika dakika ya 90.

Goli la Uruguay lilifungwa kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Edinson
Cavani katika dakika ya 24.


Nayo Uingeleza imekubali kichapo cha goli 2-1 kutoka kwa Italy katika
mchezo wa pili wa kundi C, linalo ongozwa na Coastarica.

Hadi wanakwenda mapumziko walikuwa sare ya goli 1-1, Italy walikuwa wa
mwanzo kupata goli katika dakika ya 35 kupitia kwa Claudio Marchisio.

Uingeleza iliwachukuwa dakika mbili kulisawazisha goli likifungwa na
Daniel Sturrige katika dakika ya 37.

Mario Balotelli ndiye aliyeifungia Italy goli la ushindi katika dakika
ya 50 na kuifanya uingeleza ishike nafasi ya 3 huku ya kwanza na pili
ikishikiliwa na coastarica na italy na ya mwisho ikienda kwa uruguay

0 comments