Ivory coast imewadhihirisha waafrika kuwa wanaweza kuvuka katika hatua
ya makundi baada ya kuwachapa mabingwa wa bara la Asia Japan goli 2-1.
Katika mchezo huo wa pili wa kundi D, Japan walikuwa wa mwanzo kupata
goli kupitia kwa Keisuke Honda katika dakika ya 16 na kuipeleka Japan
mapumziko wakiwa mbele kwa goli hilo moja.
Kipindi cha pili kilikuwa ni kipindi cha Ivory coast kujikusanyia
point tatu kufuatia magoli mawili yaliyotiwa kimiani ndani ya dakika
2.
Goli la kusawazisha lilifungwa na Wilfried Bony katika dakika ya 64,
na Gervinho akishinda goli la ushindi katika dakika ya 66, na kuifanya
Ivory coast kuibuka na ushindi wa goli 2-1.
Kundi D linaongozwa na Colombia ikifuatiwa na Ivory coast huku Japan
na Greece wakishika nafasi ya 3 na ya 4.



0 comments