Saturday, 11 October 2014

NATURE KUANDA KITABU CHA HISTORIA

MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya nchini, Juma Kassim ‘Sir Nature’ amesema yupo katika mikakati ya kuandaa kitabu cha historia ya maisha yake ambayo anatarajia kuisambaza hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Sir Nature, ameamua kufanya hivyo kutokana na mambo mengi aliyoyafanya katika tasnia hiyo ambayo atahitaji kumbukumbu hapo baadae.


Alisema hadi sasa yupo katika hatua za mwisho za kupiga picha baadhi ya matukio ambayo yatakuwepo katika historia yake hiyo na kuomba mashabiki wake wakae mkao wa kula kukipokea kitabu hicho kitakacholezea historia ya maisha yake tangu anazaliwa hadi kuingia kwenye muziki.

0 comments