Tuesday, 21 October 2014

KATIKA UISLAM: MWANAMKE KUTUMIA JINA LA MUME

Shukrani zote zinamstahiki Allah, Mola mlezi wa viumbe wote. Rehma na amani zimshukie Mtume (ﷺ), ali zake, masahaba wake na wale wote wenye kufuata mwenengo wake mpaka siku qiyama.
Ni utamaduni wa magharibi kwamba mwanamke akishaolewa basi hubadili nasaba yake na kujiita jina la mume. Yaani kama mume anaitwa John na Mwanamke alikuwa anaitwa Esther William, basi baada ya ndoa huanza kujiita Esther John. Kwa bahati mbaya baadhi ya waislamu bila ya elimu wameiga utamaduni huu.

Utamaduni huu ni kinyume na mafundisho ya Uislamu. Kwani Mtume (ﷺ) ameweka wazi kuwa wenye kufanya hivi wamelaaniwa, hadithi hii ni ushahidi wa laana hiyo:

قال النبي صلى الله عليه وسلّم : مَنْ انْتَسَبَ إِلَى غَيْرِ أَبِيهِ .. فَعَلَيْهِ لَعْنَةُ اللَّهِ وَالْمَلائِكَةِ

وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ " . رواه ابن ماجة 2599 وهو في صحيح الجامع 6104 والله الموفّق
Amesema Mtume (ﷺ) yoyote atakayejipa nasaba isiyo ya baba yake… juu yake ni laana ya Mwenyezi Mungu na Malaika na watu wote. [Imeripotiwa na Ibn Maajah, Hadithi ya 2599 na pia Sahihi al Jami’i, Hadithi ya 6104]

Hivy basi kama ilivyoeleza hadithi hii, kubadili nasaba ya baba ni kujitia katika laana ya Mwenye Enzi Mungu. Hili si jambo la kufanyiwa maskhara, wala si jambo la kuiga.

Na Uislamu haukukataza kubadili nasaba kwa mke aliyeolewa bali hata mtoto wa kulea (adopted child) basi pia imekatazwa kubadili nasaba yake halisi kwa ubini au ubinti wa mlezi aliyemchukua. Mwenye Enzi Mungu anatueleza katika Qur’aan kuhusu watoto hao tunaowachukua na kuwalea:

ادْعُوهُمْ لِـَٔابَآئِهِمْ
هُوَ أَقْسَطُ عِندَ ٱللَّـهِ
Waiteni kwa baba zao, maana huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. [Qur’aan 33:5]

Hivyo waislamu tusiuwache uadilifu huu kwa kuiga tamaduni zisizo zetu, tukumbuke kuwa Uislamu ni mfumo kamili wa maisha hivyo basi kila jambo lina muongozo wake katika dini hii.
A

0 comments