Wednesday 22 October 2014

DAVIDO AIWEKA LAWAMANI WIZARA

By    
 http://freemedia.co.tz/daima/wp-content/uploads/2014/10/fiesta.jpg
JEURI ya waandaaji wa Tamasha la Fiesta kukaidi amri ya Mahakama na kumpandisha jukwaani msanii maarufu wa nchini Nigeria, David Adedeji ‘Davido’ ilitokana na nguvu ya Wizara yenye dhamana na michezo, imebainishwa.

Kutokana na hali hiyo, Kampuni ya Times FM na Times Promotions and Entertainments ambao walifungua kesi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, ambako mbali na shauri la msingi, waliomba zuio msanii huyo asitumbuize siku hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Times FM, Rehure Nyaulawa, Oktoba 17 muda mfupi baada ya kutoka mahakamani aliitwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, bila kuambiwa sababu za wito huo.

“Tulishauriana na wenzangu lakini nikahisi ni kuhusiana na suala la Davido… na kweli nilipofika nikakuta ni kikao cha usuluhishi ambapo alikuwepo wakili wa Davido, Paul Mgaya, Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ruge Mutahaba, wakili wa Prime Times Promotions, wajumbe wa kamati ya utoaji vibali, wakati Mwenyekiti wa kikao alikuwa Prof. Mwasyoka, ambaye tunamfahamu zaidi kama Mwenyekiti wa kamati ya vibali,” alisema.

Nyaulawa, alisema hata hivyo mazungumzo yalionyesha wazi kulalia upande wa pili, yakiitaka zaidi Times FM na Times Promotions kuwaacha Prime Time Promotions na Davido kuendelea na shoo ya Fiesta.

“Baada ya kuona hivyo, niliwasilisha amri ya zuio iliyotolewa na Mahakama ya Kisutu na kumuomba Mwenyekiti na wajumbe wote waliokuwepo kwenye mkutano huo, kupitia nyaraka hizo ili kujionea uhalali wa kuendelea kusuluhishana kinyume na agizo la Mahakama.

“Hata hivyo wote mlishuhudia na vyombo vya habari kuripoti kuhusu zuio la mahakama, lakini Prime Time walimpandisha jukwaani na kutumbuiza licha ya kuwepo amri ya mahakama na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), kutotoa kibali,” alisema.

Nyaulawa, alisema msimamo wao ni kusimama kidete na sheria za nchi hadi haki itakapotendeka na kuonyesha kwamba hakuna aliye juu ya sheria hapa nchini.

Chanzo cha mvutano Nyaulawa anasema kupitia kampuni yao ndogo ya Times Promotion and Entertainment, walifanya mazungumzo na kampuni inayomsimamia Davido, HKN Music ya Nigeria na kukubaliana msanii huyo atatumbuiza katika tamasha lao la The Climax, Novemba Mosi.

“Makubaliano hayo yalitufikisha kwenye hatua ya kusaini mkataba na HKN Music Julai 17 mwaka huu na ulishuhudiwa na Wakili Fulgence Massawe wa hapa Tanzania, ambapo tamasha hilo litakalofanyika Novemba Mosi kwenye viwanja vya Leaders Club, Davido ndiye atakayekuwa msanii kiongozi, kwa makubaliano ya malipo ya dola 45,000 za Marekani huku tukitanguliza dola 22,500,” alisema.

Alisema kuwa, utata wa mkataba huo ulianza Oktoba 10 mwaka huu, baada ya HKN Music kuwatumia barua pepe kuomba wavunje mkataba na watarudisha kiasi walichochukua.

“Tulipouliza sababu za kutaka kuvunja mkataba huo, walituambia kuwa wameshawishiwa Davido ashiriki tamasha la Fiesta lililoandaliwa na Prime Time Promotions chini ya Clouds Media Group, kwa sababu wamepewa ofa kubwa zaidi,” alisema.

 CHANZO: TANZANIA DAIMA

0 comments