Thursday, 6 November 2014

Dr BILAL: VIJANA CHANGAMKIENI FURSA ZA UWEKEZAJI

MAKAMU wa Rais wa Tanzania, Dk. Gharib Bilal, amewataka vijana nchini kuchangamkia fursa mbalimbali za uwekezaji kwa njia ya ubia kutoka kwa wawekezaji wa nje, ili kujitengenezea fursa za ajira zitakazowafanya watajirike.

Dk. Bilal alitoa kauli hiyo Jijini Dar es Salaam jana alipokuwa akifungua kongamano la kimataifa la siku tatu la masuala ya uwekezaji wa fedha, miradi na ubia lenye lengo la kupanua fursa za uwekezaji nchini lililoandaliwa na Taasisi za Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), wakishirikiana na Kampuni ya Kukuza Mitaji ya TMS Consultants.

“Tuna changamoto ya mitaji hasa kwa wafanyabiashara wetu, kwa hiyo tunaweza kutumia fursa hii ya uwekezaji wa hisa kama mtu una kampuni au ubunifu utaweza kujipatia mtaji wa kuiendeleza biashara yako,” alisema. 
Vijana changamkieni fursa za uwekezaji - Dk Bilal
Mwenyekiti wa TPSF, Reginald Mengi, alisema hakuna nchi itakayoendelea bila ya mitaji hata kama itakuwa na maliasili nyingi, kwani haitosaidia hadi iwe na fedha za kutosha kuendesha mali hizo.

“Kwa mfano tuna gesi hivi sasa..lakini mtu hana mtaji wa kuwekeza katika sekta hiyo, hawa wenzetu wamekuja na kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kuwekeza, kwanini tusitumie nafasi hiyo?” alihoji Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP. 


CHANZO: TANZANIA DAIMA

0 comments