Wednesday, 19 November 2014

WANAFUNZI WAPAGAWA NA MPOTO UFUNGUZI WA SIKU YA KUNAWA

MAMIA ya wanafunzi wa shule za msingi wa Manispaa ya Morogoro jana walilazimika kumzingira kiongozi wa bendi ya Mjomba Mrisho Mpoto wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya kunawa mikono duniani na siku ya matumizi ya choo iliyoambatana na wiki ya usafi wa mazingira kitaifa.

Maadhimisho ya wiki hiyo kitaifa yalianza Novemba 14 na kufikia kilele leo mwaka huu katika uwanja wa shule ya msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.

Licha ya kumzingira Mpoto, baadhi ya wanafunzi walipata fursa ya kujibu maswali waliyoulizwa na msanii huyo kuhusu hatua tano za unawaji wa mikono na kupatiwa zawadi ya fedha taslimu. 
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj0UCC6qRXlGdfFBMgJUt-OyQZ-IzzZ5YLlfxAXQAg8Fk3FxhzG1XWSKPnAeU6feDUFR9S9hOu5Zgpey71b8LY-gQtFPrszOZP973r9Cq_v8qTIQ2CYdJ-40PGKDludJcvgSpXiItQ7iDZu/s1600/37.jpg
“Wanafunzi hapa nina ‘bingo’ kwa mwanafunzi ambaye ataweza kujibu swali la hatua ngapi za kunawa mikono...jitokezeni mjinyakulie zawadi,” aliwaeleza wanafunzi waliofurika uwanjani hapo.

Wanafunzi wawili wa kike na wa kiume walimudu kujibu vyema na kwa ufasaha maswali na kuzawadiwa fedha taslimu Sh 10,000 kwa mvulana na msichana Agustina Fokasi wa shule ya msingi Sabasaba B kunyakua Sh 20,000.


CHANZO: HABARI LEO

0 comments