Tuesday, 2 December 2014

KENYA: MKUU WA POLISI AJIUZULU KWA SHINJIKIZO

By    
http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/772/amz/worldservice/live/assets/images/2014/05/27/140527154839_inspekta_wa_polisi_kenya_kimaiyo_512x288_bbc_nocredit.jpg
David Kimaiyo



Mkuu wa polisi nchini Kenya inspekta generali David Kimaiyo amejiuzulu kutokana na shinikizo dhidi yake kwa kushindwa kukabiliana na utovu wa usalama nchini.

Wakati huohuo Kenyatta amempendekeza waziri mpya wa usalama Joseph Nkaiseri kuchukua nafasi ya aliyekuwa waziri wa usalama Joseph Ole Lenku.

Rais Kenyatta alisema kuwa baada ya mazungumzo na Bwana Kimaiyo alikubali 'kustaafu' mapema kutoka kwa majukumu yake kwa sababu za kibinafsi.

Wakati huohuo waziri wa usalama Joseph Ole Lenku ametimuliwa kutoka wadhifa wake huku Rais kenyatta akimpendekeza Joseph Nkaiseri kama waziri mpya wa usalama.

Rais Kenyatta alitoa tangazo hilo wakati akihutubia taifa kufuatia shambulizi la hapo jana dhidi ya wachimba migodi 36 waliouawa na Al Shabaab mjini Mandera Kaskazini ya Kenya.

Rais pia alitangaza kuwa amekubali ombi la Generali wa polisi David Kimaiyo kuachia wadhifa wake.
Kimaiyo na Ole Lenku wamekuwa wakikabiliwa na shinikizo za kuachia ngazi kufuatia kukithiri kwa utovu wa usalama nchini.

Hatua ya kuwatimua kutoka katika nyadhifa zao wawili hao bila shaka litakuwa jambo la kuridhisha kwa wakenya wengi ambao wamekuwa wakilalamikia utovu wa usalama na kuwataka waondoshwe ofisini.

Uteuzi wa Joseph Nkaisery kama waziri mpya wa usalama ni jambo jipya kwani atakuwa mwanasiasa wa kwanza kutoka kwa upinzani kuwa ndani ya serikali.

Alipokuwa anahutubia nchi,Rais Kenyatta aliwasihi wabunge kuongeza mda wa vikao vyao vya leo ili kumhoji na kumkagua Nkaisery aliyeteuliwa kuchukua nafasi ya waziri mpya wa usalama na maswala ya ndani ili wamuidhinishe.

0 comments