Wednesday, 3 December 2014

UFAFANUZI: KUVAA NGUA YENYE MAANDISHI YA QUR-AN

Dada huyu anauliza hukumu ya Qur-aan inayoandikwa na kutundikwa nyumbani au kuvaliwa ikawa kama ni Hijaab?

Jibu

Hili halijuzu. Haijuzu kutundika Qur-aan kwa njia ya Hijaab. Hili limekatazwa na Salaf. Kauli sahihi ya wanachuoni ni kwamba haijuzu. Hata kama ni Qur-aan mtu asiitundike. Hata hivyo anaweza kusomewa Qur-aan. Hili ni jambo zuri. Ama kuhusu kuitundika haijuzu hata kama itakuwa ni Qur-aan.

Ama ikiwa [kilichoandikwa] ni kitu kingine mbali na Qur-aan, kama ushirikina na mambo ya uchawi, hili kwa makubaliano ni kwamba haijuzu. Ni herizi za kishirikina. Vinavyotundikwa au kuvaliwa vimegawanyika aina mbili:
1- Qur-aan. Hili lina tofauti. Kauli sahihi ni kuwa haijuzu.

2- Mambo ya ushirikina na ya uchawi na matamshi ya kiajabu yasiyofahamika. Hili ni haramu kwa makubaliano. Ni Shirki.

Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan

http://www.alfawzan.af.org.sa/node/15243

0 comments