Monday, 30 March 2015

UN KUENDELEA KUISAIDIA TANZANIA KUTANZUA CHANGAMOTO ZA MAENDELEO

By    
DSC_0065
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile (katikati) akiwasili katika ukumbi wa mikutano kwenye hoteli ya Hyatt Regency akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo (kulia) pamoja na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez kwa ajili ya kuzindua rasmi ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania, uzinduzi uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Nyuma yao ni Mkurugenzi wa Programu kutoka Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF), Dk. Tausi Kida.
Na Mwandishi wetu
UMOJA wa Mataifa umesema kwamba utaendelea kuisaidia serikali ya Tanzania katika kutanzua changamoto za maendeleo zinazoikumba nchi hii.
Kauli hiyo imetolewa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja huo (UNDP), Alvaro Rodgriguez wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2014 mwishoni mwa wiki.
Ripoti hiyo imeandaliwa na Taasisi ya utafiti wa masuala ya kiuchumi na jamii- ya ESRF kwa ufadhili wa UNDP na inagusia changamoto za Maendeleo .
Katika hotuba yake amesema kwamba Umoja wa Mataifa unaona juhudi za serikali katika kuwakwamua wananchi katika umaskini na kutokana na hali hiyo wataendelea kusaidia mipango mbalimbali ya maendeleo pamoja na utafiti wenye kulenga kutoa suluhu kwa changamoto za maendeleo ya wananchi.
DSC_0207
Mshehereshaji wa uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania, Taji Liundi akiitambulisha meza kuu kwa wageni waalikwa (hawapo pichani) waliohudhuria uzinduzi huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Ripoti hiyo ambayo inazungumza: "mabadiliko ya kiuchumi kwa maendeleo ya watu" imesheheni mipango mbalimbali ya maendeleo na shida zake na namna ya kukabiliana na shida hizo.
Katika utafiti huo imeelezwa kuwa pamoja na uchumi wa Tanzania kukua kwa kasi umaskini bado ni kero kubwa kutokana na kukosekana kwa uhusiano kati ya ukuaji wa kiuchumi na kufutwa kwa umaskini miongoni mwa wananchi wa kawaida.
Kuanzia mwaka 2001 uchumi wa Tanzania umekuwa ukikua kwa zaidi ya asilimia 6.
Mratibu huyo wa UN nchini amesema kwamba kutokana na kasi ya uchumi kutoenda sambamba na uchumi ndio maana UN inashirikiana na serikali kuona namna bora ya ukuaji uchumi kwenda sawa na uondoaji wa umaskini miongoni mwa wananchi waliowengi.
DSC_0209
Meza kuu Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo, Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.
Wakati huo huo serikali imesema imefurahishwa na uzinduzi wa ripoti hiyo ambayo inatumaini itasaidia katika kuboresha sera na kujibu masuala muhimu ya kukabiliana na umaskini nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dk. Servacius Likwelile katika tukio hilo la uzinduzi wa ripoti.
Alisema serikali inaamini kwamba mambo yaliyomo katika ripoti hiyo yatasaidia katika harakati zake za kukabili umaskini ikiwa ni pamoja wa mipango ya maendeleo kwa kuzingatia dira ya taifa ya maendeleo ifikapo mwaka 2025.
Tanzania inajipanga kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 ikitegemea viwanda katika uchumi wake badala ya kilimo kama ilivyo sasa.
DSC_0131
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kutoa hotuba ya uzinduzi rasmi wa Ripoti ya Maendele0 ya Binadamu 2014 Tanzania uliofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
Alisema kwamba serikali imefurahishwa na jinsi ripoti ilivyojikita katika kuainisha maendeleo ya watu na sehemu kubwa ya ushauri utazingatiwa kwa mipango mipya ya maendeleo.
Ripoti ya maendeleo ya watu ni mkakati wa serikali ya Tanzania ulianzishwa Machi 2013 kwa lengo la kutafiti namna bora ya kunasua wananchi katika umaskini wakati taifa likiendelea kukuza uchumi.
Mradi huo unatekelezwa na taasisi ya ESRF ikishirikiana na Wakala wa taifa wa Takwimu (NBS), Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa serikali ya Zanzibar na kitivo cha uchumi cha chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Mradi huo unafadhiliwa na UNDP na umejikita zaidi katika kuangalia vipaumbele katika maendeleo, mambo yanayojitokeza, fursa na changamoto.
Ripoti hii inapatikana kwenye anuani zifuatazo
DSC_0223
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile akitoa hotuba kwenye uzinduzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
DSC_0228
Pichani juu na chini ni baadhi ya wadau waalikwa wakifuatilia htouba ya mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo.
DSC_0233
DSC_0241
DSC_0201
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akisoma risala kwenye uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania uliofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
DSC_0247
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile akikata utepe kuzindua rasmi Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania uliofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia uzinduzi huo ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo (kulia).
DSC_0259
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akizindua chapisho la Kiswahili la Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania huku mgeni rasmi na Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF wakishuhudia tukio hilo.
DSC_0271
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo akizundua chapisho la kingereza la Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.
DSC_0277
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile (katikati), Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo kwa pamoja wakionyesha ripoti hiyo kwa waandishi wa habari na wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.
DSC_0290
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo (kulia), Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile (katikati) na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez wakipitia nakala za ripoti hiyo mara baada ya kuzinduliwa rasmi jijini Dar.
DSC_0297
Mgeni rasmi kwenye picha ya pamoja na wadau waliofanikisha maandalizi ya ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania.
DSC_0451
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo (katikati) akiteta jambo na Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP nchini Tanzania, Philippe Poinsot (kushoto) wakati wa kupiga picha ya kumbukumbu. Kulia ni Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Amon Manyama.

0 comments