Monday, 15 June 2015

MWILI WA MUFTI KUSAFIRISHWA KESHO MKOANI SHINYANGA

By    
Kulia ni Sheikh wa Mkowa Dar es Salaam,Alhaj Sheikh Alhad Mussa Salum akiwa na baadhi ya Masheikh waliofika Nyumbani kwa Marehen Mufti,Shabaan Issa Bin Simba Mikocheni B Jijini Dar es Salaam.(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA.)

Na Chalila Kibuda.

MWILI wa  Mufti ,Alhaj Sheikh Shaban Issa Bin Simba unatarajiwa kusafirishwa kesho mkoani Shinyanga.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata),Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam,Alhaj Alhad Mussa Salum amesema mwili wa marehemu utaswaliwa kesho katika Msikiti wa Msilimu ,viongozi mbalimbali wa dini na serikali watakuwepo.

Amesema marehem alikuwa akisumbuliwa na sukari,Shinikizo la Damu (BP)  pamoja na Figo.

Hata hivyo amesema kuwa jana (Jumapili) Mufti alifanyiwa oparesheni ya figo katika Hospitali ya TM Jijini Dar es Salaam na Mauti ya Mufti yamekuta majira ya saa moja leo.

Salum amesema marehem anatarajiwa kuzikwa Alhamis mkoani mkoani Shinyanga .


chanzo:michuzibloga

0 comments