Thursday 3 September 2015

Dr.SLAA Vs Mh. LOWASA TAFAKURI YA MSHIKAJI WANGU WA FACEBOOK

By    
Dr. Wilbert Slaa

Na Baruwani Fikirini Kocho

Leo kwenye Meza ya Magazeti huku kwetu yamebaki ya Mapenzi,Michezo na Udaku...hata Daily news nayo yamekwisha...hata ungeweka gazeti la kijapani linaloandika Siasa tungenunua!....swala Muhimu ni picha ya Slaa iwepo ili Watanzania Wapate kupima aidha unafiki wake au ushujaa wake kwa Taifa.

Naamini Laiti kama Mh Lowassa angepitishwa kule Dodoma kuwa Mgombea wa CCM basi hotuba ya DK SLAA hapo jana WANA-UKAWA ingetufaa sana na tungeipokea kwa vigere gere na vifijo kama Asset au Silaha Muhimu ya vita dhidi ya CCM na Mgombea wao!...

Na sina shaka Ngonjera yetu kuu ya uchaguzi ingekuwa vita dhidi ya "Ufisadi na Wizi".

...lakini Mambo yamebadilika ..Lowassa yupo huku....Speech yetu na Vita yetu ya Ufisadi sasa tayari imehodhiwa na CCM...upepo umebadilika...wao sasa ndo wanapayuka kuhusu Ufisadi....huku sisi ikitulazimu kukazia hapo hapo kwenye kubadili Mfumo maana hatuna tena legitimacy(uhalali) na uthubutu wa kuuimba ufisadi.....Tazama Speech ya Dk Slaa anayoirudia rudia kwa kwa miaka mingi leo imegeuka Asset ya CCM....wanajitapa mpaka wanakera!.

Ni Dr Slaa huyu huyu aliyetumia miaka minane(siku 2920) kuhubiri kuhusu ufisadi kiasi cha kuonekana Shujaa anayetaka kulikomboa Taifa kutoka kwa CCM na Madhalili wao....tukamshangilia na kumsifia Shujaa huyu na Wengi kuhamasika kujiunga na Chadema....Lakini Leo tunawezaje kuzishangaa dk zake 60 alizohubiri ufisadi? ..ufisadi ule ule,misimamyake ile ile mbele ya Press Conference?

Rejea..Septemba 15, 2007 Dr Wilbrod Slaa akisaidiana na Tundu Antiphas Lissu walipokuwa Mwembeyanga na Kutaja Mafisadi wazi wazi kwa Majina....Jina la Lowassa ndio lilikuwa Chorus.

#‪#‎DR‬ SLAA ana kosa hapa?....Nadhani tunachotakiwa kufanya ni kuendelea na Mapambano ingawa tayari tuna chongo..


Leo kwenye Meza ya Magazeti huku kwetu yamebaki ya Mapenzi,Michezo na Udaku...hata Daily news nayo yamekwisha...hata...
Posted by Baruwani Fikirini Kocho on Wednesday, September 2, 2015

0 comments