Baraza
la Mitihani la Tanzania linapenda kuwakumbusha watu wote wanaotaka
kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa(QT)
mwezi Novemba, 2014 kama Watahiniwa wa
Kujitegemea kwamba kipindi cha usajili kilichoanza rasmi tarehe 1
Januari, 2014 kwa ada ya Shilingi 50,000/=kwa
wanaojisajili CSEE na Shilingi 30,000/= kwa
wanaojisajili QT kitaishia tarehe 28 Februari, 2014.
Waombaji
wote wanasisitizwa kuhakikisha wanajisajili mapema kwa njia
ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani ya www.necta.go.tz.Kabla
ya kujisajili kwenye mtandao, waombaji wanapaswa kwenda kwenye vituo
vya mitihani kuchukua namba rejea (reference number)
zinazotolewa bure na kulipa ada ya mtihani kwa njia ya Posta
au Mpesa.
Imetolewa na:
KAIMU KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA.
Chanzo: NECTA
0 comments